Bukobawadau

MNEC JULIUS LUGEMALIRA MGENI RASMI FAINALI ZA MSAFIRI MATELPHONE (MISENYI )

Zile Fainali za michuano ya Msafiri Matelphone wale mabingwa wa kuuza  simu Original aina zote zenye warrant ya miezi  12 ziweza kufikia tamati siku ya jana April 5,2015 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kyelima - Ishunju Wilayani Misenyi kwa kuzikutanisha Timu mbili majirani zenye upinzani wa jadi ni FC Mapinduzi na Kakakuona .
 Timu ya Mapinduzi kutoka kata Ishoshi wameibuka kidedea kwa bao 1-0 dhidi ya Kakakuona wenyeji wa kata ya Ishunju Wilaya ya Misenyi
Mgeni rasmi  wa fainali hizi alikuwa  Ndugu Julius Lugemalira mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wa CCM.

 Fainali hizi zimepambwa na michi ya ufunguzi kati ya Timu za wazee wa Kata ya Ishozi na Ishunju na mashindano ya kukimbia kwa wanaume na wanawake ,Timu ya Wazee wa Ishozi wameshinda bao 1-0 dhidi ya wenzao wazee wa Ishunju
Kikosi cha Timu ya Wazee wa Ishunju
Kikosi cha Timu ya Wazee wa Ishozi
Hali halisi tayari uwanja ukiwa umejaa
 Mmoja wa Mashabiki waliohudhuria ni pamoja na Bwana Willy Bukoba Tour pichani kulia
Mtangazi  wa Mechi hii Ndugu JB (Jason Begashe) anaonyesha uzalendo wa hali ya juu wakati wa mechi hii kwa kuwajua wachezaji wote Uwanjani.
 Ndugu Newton na Ndugu Mafedha pichani ni sehemu ya Wadau walio ongozana na Msafara wa Mgeni Rasmi
 Mgeni Rasmi Ndugu Julius Lugemalira ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wa CCM akikagua timu zote mbili.
 Kikosi cha Timu ya Kakakuona (Ishunju)
Hiki ndicho kikosi cha mabingwa wa Fainali za Msafiri Matelphote msimu wa tatu Fc Mapinduzi
Mgeni Rasmi ,Viongozi mbalimbali wa Chama na Kijiji,kamati ya maandalizi ya Michuano hii katika picha ya pamoja na Wavchezaji wa Timu ya Kakakuona
Beki wa Kakakuona anatolewa nje baada ya kuumia.
 Patashika Uwanjani.
 Namna mashabiki wa soka walivyomiminika uwanja
 Katika hili na lile wanaonekana Sehemu ya washabiki wa soka
Macho ya wapenzi wa soka Uwanjani.
 Ndugu Thomas Charles 'Katikilo' katika picha na Ndugu Denis Mushaijaki kamisaa wa mchezo huu.
 Mchezaji wa Fc Mapinduzi mwenye uwezo mkubwa na mwenye kasi ya aina yake
 Mwamu  anaingilia kati kuwatuliza wachezaji
Mshambuliaji Yassin Habibu wa Timu ya Mapinduzi ,akishangilia bao lake lililopatikana mnamo dakika ya 80  alilifunga kwa juhudi binafsi , Mapinduzi 1-0 Kakakuona
 Sehemu ya mashabiki wa FC Mapinduzi wakishangilia bao lao
Muauzi na kipenga chake Uwanjani
Amsha amsha pichani ni kundi la mashabiki wa Fc Mapinduzi
Mashabiki wa Mapinduzi katika kuungana na timu yao
Katika picha baadhi ya washabiki wakifuatilia  mchezo huu kwa makin
Taswira mbalimbali Uwanjani.
 Mpira unaendelea kwa kasi uwanja wa shule ya Msingi Kyelima
“Mhh! hakika ni vigumu Bukobawadau kuelezea kile tulichokishuhudia Uwanjani!!
 Mlinda mlango Prasidius Rugaimukya wa FcMapinduzi akiwa chini baada ya kuokoa mpira.
 Uninja Uwanjani, mechi ikiendelea...
Mwanzo wa mbio za mita 100 kwa upande wa wanaume
 Jamaa wakichukua kasi .
Meza kuu  pichani kulia ni Ndugu Msafiri Nyema ambaye ndiye mratibu na mdhamini wa mashindano haya yajulikano kama Ligi ya Msafiri Matephone ikiwa ni msimu wake wa tatu
 Ndugu Faustin Katunzi,Mshindi wa kwanza wa kukimbia mbio za mita 100 mashindano ya 'Msafiri Matelphone' kwa upande wa wanaumea akipongezwa na Mgeni Rasmi MNEC Julius Lugemalira.
Watoto wakiwa wamepanda juu ya  mti wakifuatilia Soka.

Kwa furaha anaonekana Mshindi wa kukimbia mbio za mita 100  kwa upande wa wanawake Bi Amida Swalehe pichani kulia.
 'Chamkunengwe' hiyo ni  Style ya ushangilia kinyumbani
Mgeni Rasmi akimpongeza Bi Amida Swalehe,mshindi wa kukimbia kwa upande wa wanawake
Wadau pichani ni Bwana Erick Martin,Bi  Magreth Wilson na Mzee Gration Nyema
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia fainali za 'Msafiri Matelphone'msimu wa tatu. 
 Watu na simu zao.
 Hakika hamasa ni kubwa mno, watu ni wengi kweli kweli..!
Ni wachezaji wa  Fc  Mapinduzi
 Yote hii ni kupitia Mtandao chaguo lako wa 'Bukobawadau' muhumi kujuwa kwamba unaweza kutatangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi pia usisahau kulike ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya /click neno hili>> >>BUKOBAWADAU MEDIA 
Sehemu ya mwisho wanaonekana Wadau wakimpongeza na kushukuru MNEC kwa kujitolea muda wake na kukubali kushiriki nao.
Nyumbani kwa Bwana Msafiri ,Ndugu Julius Lugemalira anakutana na wadau kuzungumzia kuhusu maswala  mbalimbali ya kimaendeleo.
Ndugu Newton J. Kataraia akitoa neno
Matokeo zaidi ya picha 100 tembelea ukurasa wetu wa facebook kupitia link> BUKOBAWADAU MEDIA 
Next Post Previous Post
Bukobawadau