Bukobawadau

VUGUVUGU UCHAGUZI MKUU 2015:BW.RODERIK LUTEMBEKA AWEKA WAZI NIA YA KUGOMBEA JIMBO LA MULEBA KUSINI KUPITIA (CHADEMA)

Pichani ni  Katibu wa baraza la Wazee (Chadema ) ngazi ya Taifa Bw. Roderik Lutembeka akiongea na wa kazi wa Mji Mdogo wa Muleba katika mkutano wake wa kwanza uliofanyika jana Apr 18,2015 katika Uwanja wa Red Cross Muleba.( Picha na sehemu ya video)
"Jioni ya leo nipo mbele yenu wananchi ya Muleba natangaza nia yangu ya kutaka kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hili la Muleba kusini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)"ni maneno ya Bw. Roderik Lutembeka
Nia na sababu ya kugombea kwanza ni ,kushirikiana na wananchi wa Muleba kuongeza kasi ya kusambaza huduma za kijamii katika sekta  ya afya, maji, uchumi na kushughulikia Maswala ya ardhi zinazoporwa na wenye nyadhifa Serikalini.," alisema na kufafanua zaidi juu ya rasilimali na mfumo wa Elimu 
 Bwana Lutembeka anaendelea kwa kuwahasa wananchi wa Tanzania na hasa waishio Jimbo la Muleba Kusini kutofanya makosa makubwa tena ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kimepoteza uhalali wa kuwa chama cha siasa na hakistahili tena kuiongoza serikali.
Amesema hakina uhalali kwa sababu kimeshindwa kuisimamia serikali na kusababisha vigogo wa serikali kuwatambia wananchi pale wananchi wanapotaka kuhoji matumizi ya fedha za umma.

Aidha, bwana Lutembeka amesema, nchi hii ikiendelea kuongozwa na chama hiki kuna uwezekano mkubwa wa kutumbukia kwenye machafuko kutokana na 'gepu' kubwa lililopo kati ya walio nacho (ambao kwao mabilioni ni sawa na vijisenti tu na ya kwamba kwao milioni kumi ni hela ya mbogamboga tu) na wasio nacho (ambao kwao kupata mlo wa siku moja ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu)
Akiongea kwa hekima na busara Bwana Lutembeka amejikita zaidi katika rasilimali  kama zao la kahawa,uvuvi wa Ziwa Victoria na Ardhi. 
Bw.Lutembeka amesema kuwa kinachohitajika ni Wananchi kupaza sauti kudai haki ya umilikaji wa ardhi kwa usawa na kuwekeza ndani ya ziwa ili kujipanua kiuchumi.
 "Nchi inaelekea pabaya taifa letu limekumbwa na Ufisafi mkubwa rushwa kila sekta na mambo mengine mengi,tunahitaji sasa Utawala bora"alisema
"Utawala bora unaielekeza jamii iendeshe mambo yake kwa kuzingatia, misingi ya uwazi, mapambano dhidi ya rushwa, uwajibikaji, uadilifu, ushikishwaji, utawala wa sheria, demokrasia, usawa, uhuru wa vyombo vya habari,”ni maneno ya Bwana  Roderik Lutembeka
 Amesema kwa mujibu wa historia, nchi nyingi zilizoingia kwenye machafuko ni pale ambapo kulitokea matabaka ya walio nacho na wasio nacho. Walio nacho hupata kwa kuwanyonya wasio nacho ndipo uvumilivu kwa wasio nacho hufikia mwisho na hapo ndipo binadamu huuvaa unyama na kuasi mfumo. Umma unapochoka kuvumilia ndipo kile kinachoitwa 'civil disobedience' hutokea. Mifano hipo mingi, kwa uchache ni Tunisia, Libya, Misri, Liberia n.k
 Bw.Lutembeka amewaomba wananchi kuizika CCM kwa kile alichodai ni chama kilichokwisha kufa kinasubiri maziko yake mwezi October, mwaka huu.
 Amesema dalili/ishara za chama kilichokufa hakiwasikilizi tena wananchi, kinawadhihaki. Vilevile kinatumia vijana wake wasio na nidhamu kuwapiga Wazee wanaokikosoa na hatimaye vijana wakisha fanya kazi hiyo wanazawadiwa vyeo kama ukuu wa wilaya.
Amesema pia, chama kilichokufa kinatumia vyombo vya dola kujihakikishia kusalia madarakani. Pia kinatesa na kupanga mbinu ovu za kuua wapinzani wake.
Amewaomba watanzania wote kukizika rasmi chama hiki kama walivyoweza kufanya wananchi wa Nigeria, Kenya, Malawi, Zambia na kwingineko ambako vyama vilivyojizeekea na kusahau wajibu wake kwa umma vimezikwa!

 Wadau wa mji mdogo wa Muleba wakimsikiliza mtoa nia  jimbo la Muleba Kusini.
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Bw. Roderik Lutembeka
PITIA SEHEMU YA VIDEO HAPA CHINI (FULL HD)
Kama inavyo onekana kupitia Video hapo juu, Bw. Rodeick Lutembeka akiongea kwa hekima na busara, kwa weledi mkubwa sambamba na utashi wa kisiasa kwa ajili ya ustawi wa jamii.
 Mzee Bernard Pangani Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya muleba akiongea na wanachi katika mkutano wa nia kutoka kwa Bw. Roderik Lutembeka.
 Mh.Julius Rwekyendera , Diwani wa Kata ya Gwanseli (CUF)
Katibu wa Chadema Wilaya ya Muleba BW. Elisha Kabombo akihitimisha rasmi mkutano huo
Kamanda Muongozaji wa shughuli hii pichani
 Kushoto ni Bi Joanmay Rwegasira Diwani Viti maalum Jimbo la Muleba Kusini
 Ndugu Julius Benedicto Mwenyekiti serikali ya Kijiji Makarwe na Mjumbe wa Kamati tendaji ya jimbo la Muleba Kusini.
 Haya ndiyo yaliyojiri katika Mkutano wa Mtoa nia jimbo la Muleba Kusini Bw. Roderik Lutembeka

Next Post Previous Post
Bukobawadau