Bukobawadau

MH.AMANI ANENA KWA UJASIRI KATIKA HAFLA YA WAGENI KUTOKA NYKOMBING MORS

Mh. Anathory Amani akiongea katika katika hafla fupi ya Chakula cha jioni iliyoandaliwa kwa ajili ya Wageni kutoka Nykombing Mors nchini Denmark,hafla iliyofanyika eneo la wazi ,Bukoba Corp Hotel  tarehe 5.5.2015.
Tangu kuanzishwa kwa mji huo Nykombing Mors mwaka 1983 nchini Denmark ,  uliazishwa pia  urafiki na ushirikiano wa karibu na Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba na kuanza kushirikiana katika nyanja mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo.
 Mh.Amani anasema alivyoweza kuongoza msafara wa Madiwani, Wataalam wa na Bendi ya KAKAU kwenda  Nykombing Mors nchini Denmark kuhudhuria sherehe za kusherekea mji wa Nykombing Mors kutimiza miaka 30 mwezi Juni 2013 tangu kuzishwa kwake 1983.
 Mh. Amani anasema kutokana na ziara hiyo ambayo inaonyesha ushirikiano mkubwa kati ya nchi hizo mbili,Manispaa ya Bukoba ilipatiwa gari moja la zima moto kwa ajili ya kutumika kuzima na kuepusha majanga ya moto katika mji wa Bukoba na viunga vyake ambapo,Aidha Mh,Amani anasema licha ya kukabidhiwa funguo za gari hilo wakati wa ziara hiyo pia aliomba gari jingine la wagonjwa (ambulance) na na kuahidiwa kuwa litafika mwakani 
Pamoja na kuongea mambo mbalimbali ya kuendeleza mji wa Bukoba pia Mh. Amani ameongelea hali ya kisiasa Mjini hapa na kuahakikishia Wageni na wadau waliohudhuria kwa Ujasiri kasema maneno haya;''Uchaguzi mkuu unaokuja ndio utakao amua mustakabali"..... "Nakwenda kusimama msiwe na Wasiwasi" ( kama anvyosikika katika Video na Audio sehemu inayofuata kwa  chini)
Mwenyeji wa wageni hao Mzee Johanssen Lutabingwa pichani ambaye ndiye 'Secretary Bukoba Sistership  Promotion Trust Fund' akitoa neno katika  hafla ya chakula cha jioni iliyo andaliwa na Mh.Anatory  Amani kwa ajili ya Wageni kutoka Nykombing Mors nchini Denmark.
 Mrs Anne Mette ambaye ndiye kiongozi wa Ugeni huo (Chairperson -Social Worker)akikabidhi sehemu ya zawadi walizo mletea Mh. Anathory Amani.
  Zawadi nyingine zimetolewa kwa ajili ya Mke wake na Mjukuu wake ajulikanae kwa jina la Chartte.
 Sehemu ya waalikwa wakipata huduma ya Chakula.
BUKOBAWADAU  BILA KUONGEZA NENO WALA KUPUNGUZA TUNAKUFIKISHIA HABARI HII IKIWA KATIKA SAUTI 'AUDIO ' NA VIDEO FULL VERSION
Hafla ya chakula cha jioni iliyo andaliwa na Mh.Anatory  Amani kwa ajili ya Wageni kutoka Nykombing Mors nchini Denmark ikiwa inaendelea hafla hiyo imehudhuliwa na wadau mbalimbali ,wafanyabiashara na viongozi wakiongozwa na Mwenyeji Mr. Johanssen Lutabingwa ambaye ndiye Secretary Bukoba Sistership  Promotion Trust Fund.Sistership  Promotion Trust Fund.
                 SIKILIZA YALIYOJIRI KATIKA VIDEO H HAPA CHINI 

IPATE KATIKA MP3 AUDIO HAPA CHINI  BONYEZA KITUFE CHA PLAY SEHEMU YA JUU KUSHOTO KUSIKILIZA 
Muendelezo wa matukio ya picha katika hafla hiyo.
 Ndg Rugeiyamua  ambaye ni Afisa Utamaduni Manispaa ya Bukoba katika utambulisho
Mr. Conni Mark kutoka  Nykombing Mors nchini Denmark (pichani kushoto)akitoa ujumbe wake huku Mr. Amani  akitafsiri neno kwa neno kwa lugha ya kiswahili.
Pichani kutoka kushoto ni Ndg Siraji Kichwabuta, Ndg Lawrence Barongo na Mr Victor Sherejei.
 Pichani anaonekana Mr. Charles Matunda.
 Mr Conni Mark akitoa neno na kumshukuru Mh. Amani kwa mapokezi mazuri.
 Katika utambulisho ni Mr Haus Jorgen Fink kutoka Nykombing Mors nchini Denmark
Sehemu ya waalikwa katika hafla hiyo.
 Mdau Denis akibadirishana mawazo na mmoja wa Waalikwa katika hafla hiyo.
Mtoto Chartte Mjuu wa Mh. Amani ambaye kwa namna moja ama nyingine amekumbukwa na kuletewa zawadi kutoka Nykombing Mors.
 Mr. Novatius, Mr.William Rutta ,Mdau Christopher na Mr. Medad pichani wakibadilishana mawazo
Next Post Previous Post
Bukobawadau