Bukobawadau

WAHITMU WA MAFUNZO YA SHERIA ZA USALAMA BABARANI WAMSHUKURU MAMA TIBAIJUKA

Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Tibaijuka akiongea na Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda walio hitimu mafunzo ya sheria za usalama barabarani ambapo amewataka kuwa makini  pindi wawapo barabarani ili kujiepusha na ajali.
WAHITIMU wa mafunzo ya sheria za usalama barabarani  kutoka   jimbo la Muleba kusini Mkoani Kagera wamelitaka jeshi la polisi  kuelimisha zaidi bodaboda madhara ya kuvunja sheria ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea
Wakisoma risala ya kuhitimu mafunzo hayo jana yaliyoanza April 27 mwaka huu wamesema katika mafunzo yao waendeshaji vyombo vya moto walikuwa 422 kati yao  wanawake watatu waliojifunza  sheria na matumizi bora ya barabara,Mwenyekiti wa  wahitimu hao  Bwana Sildion Bushaijabwe amesema kabla ya mafunzo ya kutambua sheria na matumizi ya alama za usalama barabarani  waendeshaji wa vyombo vya moto walikuwa wakitengeneza mazingira ya uadui na askari polisi

Bwana Bushaijabwe amesema matukio ya ajali maeneo mengi nchini yanasababishwa na  uzembe, woga wa kukutana na askari wa jeshi la polisi wakiwa  katika shughuli  za kawaida na kwamba hali hii ilivunja mahusiano yao  na bodaboda hao
Aidha wametoa shukrani kwa mbunge wa jimbo hilo Profesa Anna Tibaijuka kuwapatia ufadhili wa mafunzo hayo na kwamba kwa sasa wameondoa hofu ya kukutanana askari polisi wakiwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao
Kwa pande wake Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Kagera   Wiston Kabantega   amewahakikishia vijana hao  kuwafanyia mchakato wa kuhakikisha waendesha pikipiki  wanapata leseni na kufanya kazi kwa uhuru,Amedai kuwa pamoja na mafunzo hayo  waliopata vyeti ni washiriki 408 na wengine 48 wameshindwa mitihani na kukosa sifa za kutafutiwa leseni na kwamba vijana 14 walitoroka mafunzo  na kukosa fursa za kupata vyeti na ujuzi wa sheria
Amesema  wilaya ya Muleba imebainika kuwa na  na madereva 60 wanaoendesha magari na pikipiki zaidi ya miaka 20 iliyopita bila kuwa na leseni na hao mara nyingi wamekuwa wakisababisha ajali kwa uzembe ulevi na mwendo kasi
Pamoja na hayo vijana  hao wamesisitizwa kuhakikisha wanabeba abiria mmoja katika pikipiki na kuwa na kofia maalum ya usalama wa vichwa  vyao na abiria ili kuchukua tahadhari mara kukitokea hitilafu ya chombo katika safari zao.
Profesa Tibaijuka amesema chanzo kikubwa cha ajali kimekuwa ni mwendo kasi , kutozingatia sheria za usalama barabarani na kutotambua matumizi ya alama jambo ambalo  linatakiwa kufikia tamati na kuendesha vyombo hivyo kwa usalama zaidi ndani na nje ya jimbo hilo
Next Post Previous Post
Bukobawadau