Bukobawadau

KINANA NA MSAFARA WAKE WAHANI MSIBA WA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA BUKOBA

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mzee Samuel Luangisa
Katibu Mkuu na msafara wake waenda kuhani msiba wa Marehemu Samuel Ruangisa uliotokea siku ya jumatatu Mei 25, 2015 saa tano asubuhi jijini New York.
Mzee Samuel N. Luangisa ni mzaliwa wa Bukoba na mmoja kati ya waasisi wa TANU na hatimaye CCM, ambaye alipata kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa baada ya uhuru (1961–1964).
Mzee Luangisa ni miongoni mwa watu waliopendekeza jina la Mkoa wa Kagera badala ya jina la awali la Mkoa wa Ziwa Magaharibi.

Kinana akimfariji mjane wa marehemu Mzee Samuel Luangisa.
 Jina hilo lilibadilishwa na kuwa “Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera”chini ya ushauriano wa Mzee Luangisa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa mapema ya leo Jumamosi Juni 6,2015
 Luangisa alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM kwa muda mrefu, na baada ya hapo ameendelea kuwa Diwani wa Kata ya Kitendaguro anakozaliwa hadi 2014.
Sehemu ya Wanafamilia ya Marehemu  Mzee Samuel Luangisa
 Mr Benny Man Mulokozi na Mr Sued Kagasheki katika hili na lile.
 Mr Deo (katikati) mmoja wa wadau aliyeongozana na Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana, pichani kulia ni Mr Hamim Mahmudu Omary ,Katibu mwenezi CCM Mkoa.
 Muda Mchache kabla ya kuelekea Msibani.

Next Post Previous Post
Bukobawadau