Bukobawadau

YALIYOJIRI WAKATI PROF LIPUMBA ANACHUKUA FOMU LEO

Prof.Lipumba amechukua fomu ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ticket ya CUF/UKAWAkugombea urais leo
Prof. Ibrahim Lipumba Anasema;
=Haki?
=Haki sawa kwa nani?
=Asiependa haki?
Wanaumeeeeeeeeeeeeeeeeeeee??,
Wanawakeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ee??,
CCM!!..Kwisha kwisha kabisa, nyang'anyang'a, ndembwe ndebwe, mlalo wa chali kifo cha mende .Asanteni sana.
=Nawashukuru wote mliokuja.
(Anaonyesha picha ya wasisi wa TANU iliyopigwa 1957. MMoja wa hao wazee waliopo kwenye hiyo picha leo yupo hapa Ukumbini).
=Nachukua fomu kwa mara ya tano kwa sababu;
1. Kuhakikisha tunapata Katiba mpya. Hili jina la (UKAWA)Umoja wa Katiba ya Wananchi mimi ndo nlilibuni. UKAWA ni ummoja wa vyama vilivyo sajiliwa.
2.Nina uwezo na nia ya kuwaondosha hawa mafisadi ambao badala ya kua jela wanachukua fomu ya kugombea urais wa CCM. Wanahitajika kuwa jela na mali zao zirejeshwe
-Kidato cha tano nlisoma masomo ya hesabu uchumi na Geografia. Na chuo nliweka rekodi ya kufaulu Vizuri ambapo chuo kiliniomba nibakie shuleni nafundisha.
-Nilienda Marekani kusoma na Kurudi kufundisha chuio kikuu cha Dar. Nilikua mshauri wa Mwinyi katika maswala ya Uchumi
-Nlichaguliwa kua mshauri wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa katika maswala ya uchumi.
-Bunge la marekani walinikaribisha niwafunde kwanini nataka madeni ya Afrika yafutwe.
Bunge la Marekani nlikaribishwa kuwashauri kuhusu mahusiano kati ya shirika la fedha na Afrika. Ushauri ulikubaliwa. Nmefanya ushauri wa Wizara ya fedha Namibia, Swazland, Uganda. Katika maswala ya Ushauri nmefanya kwa muda mrefu.
Unapozungumzia maswala ya Uchumi nayaelewa sana.
-Umasikini wa Tanzania unasababishwa na Siasa mbovu za Seikali ya CCM.
-Nliulizwa umeoa? Ninaye mmoja ambaye anafanya kazi Umoja wa Mataifa ambapo yeye haruhusiwi kufanya shughuli za Kisiasa. Hata hivo mimi ndo nagombea urais sio familia ndio inagombea. Kama anataka siasa aingie kwa uwezo wake sio aingie kwenye ubawa wa mume au mke.
-Tunahitaji wakina mama waingie kwenye siasa kwa uwezo wao sio kwa kofia za familia kama ngazi. Hata Nyerere kwenye shughuli kubwa ulikua humuoni Mama Maria. Lakini sasa hivi wanabeba na familia zao.
3. Nataka wakina mama na Watoto wapate lisha bora na huduma za Msingi za Uzazi kwa kila Mtanzania. Watoto wanazaa wakiwa watoto, watoto wamedumaa, watoto wapewe Fursa za kusoma. Jambo la kuwekeza kwa watoto ndo msingi Imara
4. Kumaliza tatizo la ajira. Geografia yetu ni nzuri ambayo ninzuri katika kujenga ajira. Mtwara kuna badari asilia ya kina kirefu. Hapo kuna fursa ya Biashara kwani kuna gesi, Tanga kuna bandari na kunakubali kila aina ya mazao. Vilevile sekta ya kilimo ni sehemu nzuri sana ya kutengeneza ajira.
=Ujenzi wa miundo mbinu imara, sio tu tunaongeza ajira bali usalama pia kwani nchi nane tulizopakana nazo zinategemea bandari za Tanzania.
5. Hali ya Afya. Tunatakiwa tuwe na hifadhi ya jamii kwani wazee wanateseka kwa kuwa hakuna huduma.
6. Ufisadi. Kama nikichaguliwa kupeperusha bendera ya UKAWA, sitakuwa na huruma na mafisadi
=Kama UKAWA watanipendekeza kupeperusha bendera, Nikiwa rais ntaunda Serikali ya Umoja wa kitaifa kupambana na ufisadi.
=Nipo tayari Kumuunga mkono na Kumpigia debe Mgombea yoyote ambaye atapitishwa ndani ya UKAWA. Ninacho waomba wananchi, Nendeni kujiandikisha ili tupige kura na kulinda kura pia, kwani miaka ya kuchakachuliwa imeshapitwa na wakati. Asanteni sana.
Kamaliza kuhutubia 15:15GMT
Asanteni.
Next Post Previous Post
Bukobawadau