Bukobawadau

KATIBU TAWALA MKOA WA KAGERA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA WAGONJWA MAHUTUTI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA

Kati ya majukumu makuu manane ya Sekretarieti ya Mkoa jukumu mojawapo kuu ni Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi, jukumu ambalo linaisogeza serikali kuu karibu na wananchi wake kwa mkoa husika.
Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera inayongzwa na Mtendaji Mkuu wake  Katibu Tawala wa Mkoa  Bw. Nassor Mnambila pamoja na kutekeleza majukumu yote manane kwa wananchi wake lakini jukumu la kutekeleza shughuli za maendeleo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi analitekeleza ipasavyo.
 Kutokana na ukuaji wa kiuchumi unaosababishwa na kukua kwa ongozeko la watu katika mkoa wa Kagera vilevile huduma za kijamii zinahitajika kupanuliwa ili kukidhi ongezeko hilo jambo ambalo lilimfanya Bw. Nassor Mnambila kuamua kujenga wodi ya wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit) katika Haspitali ya Rufaa Mkoa Kagera.
 Kutokana na ukuaji wa kiuchumi unaosababishwa na kukua kwa ongozeko la watu katika mkoa wa Kagera vilevile huduma za kijamii zinahitajika kupanuliwa ili kukidhi ongezeko hilo jambo ambalo lilimfanya Bw. Nassor Mnambila kuamua kujenga wodi ya wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit) katika Haspitali ya Rufaa Mkoa Kagera.
Aidha akiongea na uongozi wa hospitali hiyo Bw. Mnambila alitoa changamoto kwao kuwa sasa ni wakati wa serikali kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayowagusa wananchi moja kwa moja badala ya kuitegemea serikali tu ambapo aliwashauri kuandika maadiko ya miradi mbalimbali na kuiuza kwa sekta binafsi na mashirika yasiyokuwa ya serikali.

Kutokana na maeneo ya hospitali hiyo kuonekana kuwa finyu kwasababu ya kujenga majengo mbalimbali ya chini aliwashauri kuona uwezekano wa kujenga majengo ya kwenda juu ambayo ni maghorofa kwasababu itafika mahali hakuna tena sehemu ya kujenga jengo lolote kutokana na ufinyu wa ardhi.

Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Thomas Rutachunzibwa akimshukuru Katibu Tawala Mkoa Bw. Mnambila alisema anamshukuru yeye binafsi na serikali kwa ujumla kuona umuhimu  wakujenga jengo la wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa na kupunguza usumbufu waliokuwa wanaupata, lakini mara baada ya jengo hilo kukamilika litaondoa tatizo hilo.

Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera inawahudumia wastani wa wagonjwa 12,000 kwa mwezi na wastani wa wagonjwa 150,000 kwa mwaka ambapo mwaka 2013 iliwahudumia wagonjwa 151,915 na mwaka uliofuata iliwahudumia wagonjwa 156,376. Lengo kubwa la Sekretarieti ya mkoa wa Kagera ni kutoa huduma nzuri kwa wananchi wake.
Next Post Previous Post
Bukobawadau