Bukobawadau

SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KITUO CHA POLISI SITAKISHARI ZAKAMATWA, KATIKA MAPAMBANO, MAJAMBAZI WATATU WAUAWA, WAWILI WAKAMATWA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
20/07/2015
SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KITUO CHA POLISI SITAKISHARI ZAKAMATWA,
KATIKA MAPAMBANO, MAJAMBAZI WATATU WAUAWA, WAWILI WAKAMATWA.

Oparesheni kali yakupambana na makosa mbalimbali ya uhalifu wakutumia silaha za moto inaendelea jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana kwa karibu na mikoa jirani.

Katika tukio la hivi karibuni tarehe 12/07/2015 kundi la majambazi waliokadiriwa kufikia 16 hadi 18 walivamia kituo cha Polisi Sitakishari wakati wa usiku na kisababisha vifo vya askari wanne na raia watatu pamoja na uporaji wa silaha kadhaa na risasi.

Mara baada ya tukio hilo oparesheni kali ya usiku na mchana kwa ushirikiano wa vikosi mbali mbali lianzishwa.

Matokeo ya oparesheni hiyo nikamaifuatavyo:

Mnamo tarehe 17/07/2015 zilipatikana taarifa zakuaminika kwamba huko maeneo ya TOANGOMA mkoa wa kipolisi Temeke kulikuwa na majambazi waliohusika kwenye tukio la Sitakishari wakijiandaa kufanyatukio la uhalifu.

KikosiMaalum (TASK FORCE) kiliendaeneo la tukiona kuweka mtego ilikuwanasa washukiwa.

Kutokana na taarifa zilizokuwepo askari wakikosi hicho waliwasimamisha watu watano waliokuwa wamepakizana katika pikipiki mbili lakini walikaidi kusimama na badala yake mapambano makali ya kurushiana risasi yalianza.

Watuhumiwa watano walikamatwa na watatu kati yao walikuwa wamejeruhiwa vibaya na hivyo walifariki dunia wakiwa njiani kukimbizwa hospitali.

Majina ya waliofariki ni kama ifuatavyo:

ABBAS S/O HASHIM,
Mkazi wa mbagala.

YASINI,
Mkazi wa Kitunda Kivule.

SAID,
Mkazi Kitunda Kivule/Kijiji cha Mandimkongo Mkuranga.

Watuhumiwa wawili ambao ni

RAMADHANI S/O HAMIS ULATULE,Miaka 15, Mkazi wa kijiji cha Mandimkongo Mkurangana

OMARY S/O OMARY AMOUR, Miaka 24, Mkazi wa Mbagala Kimbangulile walipatikana na kuhojiwa.

Katika tukio hilo ilipatika na bunduki moja aina ya SMG ambayo namba zake zilifutwa ikiwa na risasi 25.

Katika mwendelezo wa oparesheni hiyo kali, tarehe 19/07/2015 zilipatikana habari zakuaminika kwamba silaha zilizoporwa Sitakishari zimefichwa mkoa wa jirani wa Pwani katika sehemu isiyofahamika vizuri korini.

Katika ufuatiliaji Kundi kubwa linaloundwa na vikosi mbalimbali vya Polisi lilienda mkoa wa Pwani na kufanya msako.

Mafanikio yaliyopatikana katika msako huo ni kamaifuatavyo:

Katika kijiji cha Mandimkongo kata ya BUPU, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani katikati ya msitu/vichaka baada ya taarifa zakuaminika kikosi maalum kilifukuaardhinina katika shimo hilo zilipatikana bunduki 15 ambapo kati ya hizo Bunduki SABA (07) niainaya (SMG), bundiki SABA (7) niainaya SAR, MAGAZINE MOJA YA SMG yenye risasi 28, na zote zimetambuliwa kwamba ni silaha za kituo cha Polisi Sitakishari zilizoporwatarehe 12/07/2015.

Katika shimo hilo lililofukuli wapiailipatikana silaha moja aina ya the NORINKO ambayo inafanyiwa uchunguzi kujua wapi ilipoibiwa.

Pia katika shimo hilohilo zilipatikana fedha taslim za tanzania shilling MILLIONI MIA MOJA NA SABINI(TSHS: 170,000,000/=)ambazo zilifungwa katika sanduku maalum.

Muhtasari wamafanikio nikama ifuatavyo:

Kukamatwa kwa watuhumiwa watano ambapo watatu walipoteza maisha katika mapambano na polisi.

Kupatikana kwa silaha kumina sita ambapo kumi na nne kati ya hizo ziliporwa katika tukio la Sitakishari na mbili ni za majambazi.

Zimepatikana jumla ya risasi 53 ambapo risasi 28 niza kituo cha Sitakishari na risasi 25 ni za majambazi.

Fedha taslimu za kitanzania shillingi million mia moja na sabini (Tshs 170,000,000/=ambazozinachinguzwa.

WANAOTAFUTWA NA POLISI(WANTED PERSONS)

Oparesheni hii ni endelevu na kwamba bado inaendelea kwa ukali uleule pamoja namafanikio yaliyotajwa.

Tunahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali ilikutokomeza kundi hili la watu wachache ambalo limegundulika kuwa na tabia yakuvamia vituo vya Polisi kuua askari na kupora silaha, kupora katika taasisi za fedha, kupora kwa kutumia pikipiki(bodaboda), n.k.

Katika harakati hizo wafuatao wanatafutwa na Jeshi la Polisi haraka iwezekanavyo:

ABDULAZIZI S/O AHMAD

ABDULRASHID @ USTAADH

ABDULAZIZ anaishijijini Dar es Salaam –Kiongozi wa Kundi

SHABAN S/O MOHAMED MTUMBUKA @ AMIR SHABAN NDOBE

HANNAFI S/O JUMANNE KAPELA @ MKAMBA @ SHEIKH HANNAFI

HASSAN S/O HARUNA ISSA @ DR. SHUJAA
ZAHAQ S/O RASHID NGAI @ MTU MZIMA.

ABUBAKAR S/O NGINDO @ ABU MUHAMMAD

KHAMIS S/O RAMADHAN
USTAADH RASHID (Aliua wakati katukio la Sitakishari).

S.H. KOVA - CP.
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM YA POLISI D’SALAAM
Next Post Previous Post
Bukobawadau