Bukobawadau

MATUKIO KUTOKA MLIMANI CITY HAFLA YA WASANII KUMUAGA RAIS KIKWETE

1
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dr. Jakaya Kikwete, Kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MLIMANI CITY-DAR ES SALAAM) 3
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto, Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli na Mwigizaji Jacob Steven JB wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Diamond.
4
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanawa pili kutoka kushoto ar es salaam Mh Meck Sadik na Muigizaji Jacob Steven JB.
5
Mwanamuziki Nasib Abdul aka Diamond Platnumz akiwasili na Meneja wake wa Shughuli za kimataifa Bw.Salam.
6
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto wakati wakiigia ukumbini.
7
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto,Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli wa pili kutoka kulia na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba.
8
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto,Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli kulia na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakipiga makofi wakati wimbo maalum ukiimbwa.
9
Davis Mosha kulia akiwa pamoja na Mboni Masimba wa The Mboni Show wakiperuzi kwenye simu.
10
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Davis Mosha na Mboni Masimba
11
Rais Dr. Jakaya Kikwete akina baadhi ya viongozi wa bendi za muziki wa Taarab.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Bw. Godfrey Kusaga mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Primetime. 16
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Adam Mchomvu mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds Radio.
17
Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mtandao huu Bw. John Bukuku kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
19
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Davis Mosha kushoto ni msanii Mwana FA.
20
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wasanii mbalimbali kutoka kushoto ni Mwigizaji Jacob Steven, Mwanamuziki Jose Mara na Mwana FA.
21
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na wasanii mbalimbali kutoka kushoto ni Mwigizaji Jacob Steven, Mwanamuziki Jose Mara, Mwigizaji Monalisa aka Yvone Cherry na Mwana FA, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik.
22
Kutoka kulia ni Mama Monalisa . Juma Kaseja, Dokii na Monalisa wakiwa katika hafla hiyo.
23
Ali Choki kushoto na anayefuatia ni msanii Kitale pamoja na wasanii wenzao wakiwa katika hafla hiyo.
24
Kutoka kushoto ni Mabosi wangu Edward Mpogole, Daniel Chongolo na Juma Kengele wakipozi kwa picha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aungana na viongozi wengine baada ya kuwasili katika hafla aliyoandaliwa ya kumuaga, na kumkaribisha Mhe. John P. Magufuli.
Mgombe Urais Mhe. John P. Magufuli akimuunga mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla ya kutambulishwa na kumuaga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mhe. Nape Nnauye, Mhe. Abdulrahman Kinana, Mhe. John P. Magufuli na Mhe. January Makamba wakijumuika kwa pamoja katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Abdulrahman Kinana na Mhe. January Makamba wafika kwenye hafla maalum ya kumuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kumkaribisha Mhe. John P. Magufuli.
Mhe. John P. Magufuli akishiriki kwa kupiga ngoma akionyesha furaha kwenye nyimbo ya kumuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla.
‪#‎UmojaNiUshindi‬

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete alizungumza mambo mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa muziki pamoja na Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu kwa sasa hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani akiserebuka na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha,ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya ukumbi wa mlimani City jijini Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uuenezi Nape Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (mwisho kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Paul Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo  na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia akishiriki tukio hilo.Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali  wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dk.Jakaya Kikwete.
 Baadhi ya Wadau wa muziki wakifurahia jambo wakati Rais Dkt Jakaya Kikwete alipokuwa akiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wadau wa muziki nchini ndani ya ukumbi wa mlimani City usiku huu.
 Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom,Kelvin Twisa
 Dkt Kikwte akisalimiana na baadhi ya Wasanii wa muziki wa bongofleva
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick ndani ya ukumbi wa mlimani city usiku huu.
Wanauziki wakongwe pia walikuwepo kumshukuru Rais Kikwete kwa mambo mengi aliyoyafanya katika uongozi wake wa miaka kumi ndani ya tasnia ya muziki. 

PICHA NA MICHUZI JR.

Next Post Previous Post
Bukobawadau