Bukobawadau

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YATEMBELEA MSD


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa  Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Ukimwi, Hassna Sudi Katunda Mwilima (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe hao na wageni katika ziara hiyo.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (kulia), akiwatembeza wajumbe hao MSD Keko.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (katikati), akitoa maelekezo kwa wajumbe hao.

Na Mwandishi Wetu

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI na dawa za kulevya wametembelea Makao makuu ya Bohari ya dawa (MSD), Keko jijini Dar es Salaam.  Katika ziara yao kamati imeishauri serikali kutenga bajeti ya dawa na vifaa tiba kulingana na mahitaji. 

Akitoa ufafanuzi kuhusu asilimia 80% ya dawa kuagizwa nje ya nchi, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu amesema bado hakuna viwanda vya ndani vya kutengeneza dawa ,na vichache vilivyopo havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya MSD.

Katika hatua nyingine,wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge ya masuala ya UKIMWI,inayoongozwa na Mhe.Hassna Sudi Katunda Mwilima(Mb.) imeipongeza MSD kwa kuwa na maghala ya kisasa ya kuhifadhia dawa,huku wakihimiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ishughulikie deni la serikali. Aidha, walisema kulipwa kwa deni kutasaidia MSD kununua dawa muhimu kwa wakati.

Kuhusu deni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya alieleza kuwa suala la deni linafanyiwa kazi.

Hata hivyo Naibu Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kuwa tayari serikali imeshaahidi kupunguza deni kwa awamu kuanzia mwaka huu wa fedha.

Next Post Previous Post
Bukobawadau