Bukobawadau

Kongamano la Moyo wa Wanawake lafana

Mwishoni mwa wikiendi ilipopita kumemalizika tukio kubwa kuelekea siku ya mwanamke Duniani, kulikuwa na Kongamano la  Moyo wa Mwanamke Katika kanisa la Living Water Centre kawe,Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuwakutanisha wanawake wa kila dini,rika,rangi na wengine ikiwa ni kwa lengo la kuwakumbusha nafasi yao katika ufalme wa Mungu.

 Kongamano hilo liliandaliwa na huduma ya Wamama kanisani hapo ikiongozwa na mmbeba maono Mwalimu Lilian Ndegi kwa msaada wa mme wake Apostle Onesmo Ndegi kiongozio wa huduma ya Living Water Centre Ministry.

Kongamano hilo huwa linalofanyika mara moja kila mwaka kanisani hapo kwa kusudi la kuwajenga Wanawake kuwa na uwezo katika kumtumika Mungu na kujua nafasi yao ya kutumika nafasi aliyowapa katika ufalme Mungu.

Kongamano hilo limefanyika baraka na msaada kwa wakina mama wengi Kuombewa na  kwa kufundishwa kukabiliana na mazingira magumu na changamoto mbalimbali katika maisha kwa kujua nafasi yao Mungu aliyowapa na uwezo aliowapa kukabiliana na majukumu katika ngazi ya Familia,Huduma,Jamii na Taifa kwa ujumla.

 Kongamano hilo lilikuwa na wazungumzaji kuoka baadhi ya nchi za Afrika Mch. Salome Mushi kutoka Botswana,Askofu Angela Acha Morfow kutoka Cameroom,Mch. Jael Tengu kutoka Nairobi Kenya na Mwenyeji Mwl.Lilian Ndegi

 Waimbaji mbalimbali walikuwepo Women of The Kingdom,Living Waters,More than Enough Band na wengine wengi.

Mwenyeji Mwl.Lilian Ndegi
Askofu Angela Acha Morfow kutoka Cameroom
Mch. Jael Tengu kutoka Nairobi Kenya
Mch. Salome Mushi kutoka Botswana
Mch. Naomi Mhamba wa Living Water Center Tanzania
Wanaume wachungaji walikuwepo kuhudhulia Kongamano hilo





Wanenaji wa Kongamano la Mwanamke 2016 katika picha ya pamoja wa kwanza kushoto ni mwenyeji Mwl. Lilian Ndegi,Angela Morfaw kutoka Cameroon,Apostle Onesmo Ndegi mwenyeji,Jael Tengu kutoka Kenya na Salome Mushi Botswana.
Maombi na Maombezi kwa wenye magonjwa na uhitaji yalikuwepo
Maombi na Maombezi kwa wenye magonjwa na uhitaji yalikuwepo
Maombi na Maombezi kwa wenye magonjwa na uhitaji yalikuwepo
Next Post Previous Post
Bukobawadau