Bukobawadau

ASEMAVYO MDAU MWESIGA 'KAGERA YAGERA'

Kama kagera si wa mwisho kimaendeleo basi tuko katika nafasi ya pili kutoka mwisho. Inaumiza sana kuona mkoa uliokuwa namba moja ukishindana na KILIMANAJARO na MBEYA sasa hivi hata mikoa mipya imetutupa mbali. Kweli baadhi wana machungu ila pa kuanzia ni wapi? Je wapi kila mmoja wetu anaona gap ili liweze kuwekwa bayana? Je ni vema maoni na malalamiko yetu yakawa yanaishia kwenye blogs, or other online media? Je hamasa gani wewe na mimi tuweke? Je nini mrejesho au matokeo ya makongamanoo yaliyowahi kufanywa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya mkoa wa kagera angalau kuona mpango wa muda mfupi. 
 Labda yapo kwa mnaoishi bukoba tujulishe jamani. ABAANA BASHOME, FRIENDS OF BUKOBA, KAGERA AGENT FOR CHANGE nk wapi mipango yenu. MAANA SIJUI HATA KAMA WABUNGE WA MKOA WETU HUWEZA KUKAA PAMOJA NA KUJADILI YAHUSUYO KAGERA.. MADIWANI JE KUHUSU HALMASHAURI ZENU? Ni mapema lakini mchuzi wa…………….. hunywewa ukiwa wa moto.
 Au ni sawa na theory za wanafalsa wa zamani G. Vico 16th -17th c na Ibn Khaldun 14-15th c waliotoa CYCLIC NATURE OF HISTORY. Kwamba lazima kuwepo upside and down kuwa hatuwezi kuwa juu siku zote? Lakini je mbona Kilimanjaro wapo juu. Mbona Mbeya wanakimbia. Je ni KAMUNOBELE?
Wenzetu wa Kigoma, Geita, Singida wana utashi wa maendeleo wanawaza kwa kina kusogea mbele, mfano baraza la madiwani kigoma ujiji wna mipango mizuri sana yakimaendeleo katika sekta zote. Hyo ni ujiji tu ukijumlisha wengne wanasonga.
Wasafiri mnaona singda wanavyo come up jaman, Dodoma mbali na kuwa makao makuu ya nchi ndo usiseme. Jamani hata Tabora, Shinyanga tu mji unauzidi wa Bukoba? Achana na miji ya mikoa jaman miji ya wilaya nayo inakimbizana inatuacha mfano mzuri ni KAHAMA mtu apinge kama Kahama si zaidi ya Bukoba. Waangalie WAKURYA

Chei shana bakaturoga anga tukeroga si? Are we thinking? Viongozi mko wapi? Najua hatuwezi kuwapima kwa miez michache lkn tupe matumaini ya short term plan huku tukiandaa kwa pamoja ;long term plan. Jamii ikishirikishwa na ikawa na utashi wa kweli tutatoka tulipo. Eilanga elayabayo zamani mwaa kowakubigamba mbakusheka busha.
Je ni baadhi yetu kutokuwa na mapenzi mema na kwetu maana nshakutana na wengi huwambii kitu kuhusu nyumbani anakwambia mi kwetu Mwanza or Dar es Salaam yaan aibu tupu.
Naomba nikomee hapo ni maumivu.

 CREDIT:Mwesiga Mwesiga
Next Post Previous Post
Bukobawadau