Bukobawadau

HIJA KWA BIKIRA MARIA NYAKIJOGA:Lurdi ya Bukoba yafanyika Leo Oct 2,2016

 Waumini wa dhehebu la kanisa katoliki leo wameungana pamoja kwenye ibada ya hija ya Bikira Maria iliyofanyika kwenye eneo la Nyakijoga lililoko katika kata ya Mugana iliyoko wilayani Misenyi kuwaombea watu 17 waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na waliathirika na tetemeko hilo lilisababisha maafa makubwa ambayo ni pamoja na uharibifu wa nyumba za makazi na majengo ya taasisi za serikali.
 Askofu Kilaini: "Tetemeko la ardhi ni kengere ya Mungu ya kutuamsha (kutuzindua) tuijenge upya Kagera."
 Viongozi mbalimbali wa Kichama na Serikali wamewdha kushiriki Ibada hiyo
Baadhi wa Waumini wa Kikatoliki wakiendelea kushiriki Ibada ya Hija ya Nyakigoja iliyofanyika leo Jumapili Sep 2,2016


Kituo hiki cha Hija kilianzishwa kwa madhumuni ya kushiriki kiroho katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu tamko rasmi la Kanisa la mwaka 1854, kuwa ni nguzo ya imani kwamba Bikira Maria aliumbwa bila dhambi ya asili.
Vilevile, mwaka 1958 kuliadhimishwa Jubilei ya miaka 100 tangu Bikira Maria mwenyewe alipomtokea msichana Bernadeta Subiru huko Lurdi Ufaransa mwaka 1858 na kujitambulisha kuwa yeye ndiye “aliyeumbwa bila dhambi ya asili”
Wakati Ibada hiyo ikiendelea
Taswira mbalimbali kutoka eneo la Hija Nyakijoga Mugana
#‎Bukobawadau‬
Next Post Previous Post
Bukobawadau