Bukobawadau

HOSPITALI YA KAIRUKI KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZAKE KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WAGONJWA

Hospitali ya kairuki katika kuboresha huduma zake kwa wagonjwa imeanza kutumia kitengo kipya kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kutwa  hususani wale wanachama wa mfuko wa Taifa  wa Bima ya Afya (NHIF).
Kitengo hicho kipya (OPD 3)  kilichopo nyuma ya Jengo kuu la hospital mkabala na kitengo cha magonjwa ya viungo ( Physiotherapy Unit) kina sehemu kubwa ya mapokezi, vyumba  mbalimbali  vikiwemo  vyumba 10 via madaktari, maabara,Duma la dawa,sehemu ya sindano na kufunga vidonda,chumba cha ultrasound,mapokezi , huduma za chanjo ya watoto (RCH),chumba cha wauguzi na duka dogo la vinywaji na vitafunwa nk .
Kitengo hicho kipya kitaiwezesha hospital hiyo  kutoa huduma kwa haraka na ufanisi kwa wagonjwa  wasiopungua 120000 kwa mwaka  hivyo kupunguza Kero ya foleni na msongamano iliokuwepo siku za  nyuma.


Aidha kitengo hicho (OPD3) kitazinduliwa rasmi hivi karibuni pamoja na vitengo vipya vya kusafishia figo ( Dialysis Unit) na kile cha huduma za dharula ( Emergency Unit)

Pichani ni Majengo mapya ya kisasa yatakayokuwa yakitumika kutoa huduma.
 Pichani wagonjwa wakisubiri kupata huduma Muda  mfupi Mara baada ya majengo hayo kufunguliwa.
Pichani wagonjwa wakisubiri kupata huduma Muda  mfupi Mara baada ya majengo hayo kufunguliwa.
Na Afisa Mahusiano;Arafa Mohamed
Next Post Previous Post
Bukobawadau