Bukobawadau

SHEREHE YA JUBILEI YA KUMPONGEZA MZEE BARUTI KWA KUTIMIZA MIAKA 80 YA KUZALIWA

 Familia ya Mzee Wilson Baruti waungana katika Sherehe ya Kumpongeza mzazi wao kwa kutimiza Miaka 80 ya kuzaliwa kwake na Kuadhimisha Jubilei ya miaka 49 ya ndoa yake na Mama yao mpendwa,Mama Astedia Baruti,sherehe iliyofanyika Nyumbani kwao kijijini Burugo Dec 24,2016
Pichani ni watoto wakuzaliwa na Mzee Wilson Baruti, aliyebahatika kubata watoto 15 ,Wakiume 8 na wakike 7 ,kati yao Mwenyezi Mungu alimuita mtoto mmoja Renatha Baruti tunamuombea Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amina...
 Bwana Ruga Baruti katika picha ya pamoja na Wazazi wake Mzee Wilson Baruti na Mke wake Mastidia Baruti ambao wametiza Miaka 49 ya Jubilei ya dhahabu ya ndoa yao.
 Baadhi ya Waalikwa walioshiriki shughuli hiyo iliyofanyika Kijijini Burugo kata ya Nyakato Dec 24,2016
Tukio linalofuata ni Kukata Keki.
Kukata Keki maalum kwa ajili ya  maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 ya kuzaliwa kwake Mzee Wilson Baruti.
Mzee Wilson Baruti akiwa tayari kumlisha Keki Mke wake  Mama Mastadia Baruti
Naaam..!Siku ya kuzaliwa Mzee wetu Wilson Baruti na  jubilei ya Miaka 49 ya ndoa yake na Mke wake Mama Mastidia Baruti kama anavyo onekakana pichani akimlisha Keki Mmewe Mpendwa.
 Mdau Jumanne Bingwa pichani.
 Wajukuu wa Familia ya Mzee Wilson Baruti wakitoa Burudani
 Mzee Mwijage na Mke wake pichani wakifurahia burudani iliyokuwa ikiendelea kutoka kwa Wajukuu wa Mzee Wilson Baruti
Huduma ya Vinjwaji ikiendelea Sawa bin haki kwa watu wote Ukumbini
 Mdau Edgar Kyarusi akitoa Mkono wa pongezi
 Waalikwa wakielekea kutoa pongezi Zao.
 Mulangira Deo Deka, Mkubwa Emiry Baruti na Mpambanaji Optaty Henry (Katibu) wakibadilishana mawazo
Bi Alice Theobard kati ya waalikwa walioshiriki sherehe hiyo
 Mr Kashasha akiteta jambo na Mzee Pius Ngeze ambaye ni rafiki mkubwa wa familia ya Mzee Baruti
Shughuli ya sherehe hiyo iliyowakutanisha Wanafamilia na marafiki kutoka maeneo mbalimbali ikiwa inaendelea...
 Taswira eneo la tukio wakati sherehe ikiendelea
Zawadi nzuri ya Makochi iliyotolewa na Watoto wa kuzaliwa na Mzee Wilson Baruti
 Adv. Ishengoma akilakiwa na rafiki yake Mulangira Deo Deka mara aliwasili nyumbani kwa Bwana Ruge Baruti kwa ajili ya kushiriki hafla ya kumpongeza Mzee Baruti kwa kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa kwake.
Waalikwa wakifurahia Shughuli hiyo iliyofanyika Kijijini Bulugo-Mugeza nje kidogo ya Manispaa ya Mji wa Bukoba.
 Mjengo wa Bwana Ruga Baruti uliopo Nyumbani Kijijini Burugo Bukoba


Mama Mastidia Baruti akiwa tayari kupanda Gari kuelekea  sehemu ilipo nyumba yao ya Kimila (Mshonge) yalipo anzia maisha yao.
 Bwana Ruga Baruti akiwa tayari kuongoza na Wazazi wake na Wanafamilia kuelekea kwenye Nyumba ya asili ya Mzazi wake 'Msonge' alipoyaanzia maisha.
 Blogger Mc Baraka akipata Mawili matatu kuhusu historia ya Mzee Baruti na Nyumba hiyo ya Kimila 'Mshonge'
Katika picha ya kumbukumbu mbele ya Nyumba ya Kimila
Mara baada ya kupata baraka katika nyumba yao ya Kimila
 Wakilejea kuendelea na sherehe  rasmi iliyotanguliwa na Ibada ya Shukurani.....Endelea kuwa nasi kwa mtiririko wa matukio zaidi ya picha...
Maswala ya Nyama Choma na Misosi ya kila aina yaliweza kuhusika katika sherehe hiyo.
Inaendelea Soon......BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0768 397241

Next Post Previous Post
Bukobawadau