Bukobawadau

Wenyeviti Wawili Washikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera

MWENYEVITI wa wili wa serikali ya kijiji cha Nyabihanga na mwenyekiti wa kitongoji cha Bihanga wilayani Ngara wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu wawili wakazi wa wilayani hiyo.
 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Ollomi akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake amewataja watuhumiwa hao kuwa ni mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyabihanga bwana Eradi Batakanwa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Bihanga wilayani Ngara. 
Hata hivyo amesema kuwa, watuhumiwa  hao wamekamatwa juzi na jeshi la polisi kutokana na tuhuma zinazowakabili za mauaji ya watu wawili ambao ni Mwalimu Audax Elias (34) na Sadoki Erenesti (15)  Wote wakazi wa  wilaya ya ngara.
 
Ollomi alisema kwamba, mnamo desemba 17 mwaka huu marehemu wawili ambao ni Audax Elias na Sadoki Erenesti walifika katika kijiji cha Nyabihanga kata ya Bukiliro wilayani Ngara kwa lengo la kununua mbuzi na kuku wa biashara ndipo wananchi walianza kuwashambulia wakiwadhania kuwa ni wezi wa kuku na mbuzi.

Aidha alisema kwamba,  mwili wa sadoki umepatikana jana baada ya ushirikianao wa wenyeviti hao na mwili wa Audax unaendelea kutafutwa leo kwani  eneo la tukio wamekuta suruali yake na viatu alivyokuwa amevaa.
 
Kamanda Ollomi aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kwa wale wote waliohusika kwenye tukio hilo waweze kukamatwa kwani kuna wengine bado wanaendelea kutafutwa na jeshi  hilo.
mwisho.
Na Mwandishi wetu.
Bukoba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau