Bukobawadau

ELIMU BILA MALIPO INAHITAJI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAZINGIRA YA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA

 Wanafunzi wa shule ya msingi Nshanje kata ya Kyebitembe Wilayani Muleba Mkoani Kagera wakisomea chini ya miembe kutokana wa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo Kamera yetu imepita na kujionea hali halisi.
Pia shule hiyo haina nyumba hata moja ya Walimu licha ya kuwa na walimu 9 na iliyojengwa miaka 10 iliyopita imeishia renta huku serikali ya kijiji cha Kasindaga ikijenga ya miti ili walimu hao wapunguze kutembea umbali wa kilomita 18 kila siku kwenda kufundisha wanafunzi wa shule hiyo.
 Changamoto zinazowakabili wanafunzi wa shule hiyo pia ni vyoo wakijisaidia katika vyoo vilivyopo vya muda mfupi ambavyo vimejengwa kwa matete na kulazwa mabati huku wakihofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko
 Wanafunzi wakielekea katika Vyoo na walimu bado wanajisaidia katika mazingira hayo
Walimu wa shule hiyo na wanafunzi pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Kasindaga Mathias Bishobo wamethibitisha kuwepo wa changamoto hizo na kwamba wananchi wanajitahidi kuchangia vifaa vinavyopatikana kwenye mazingira yao ili kuboresha Miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kuiomba serikali kuchangia vifaa vya ujenzi vitokavyo viwandani
 Habari na picha kwa hisani ya  mwandishi wetu Shaaban Ndyamukama kutoka Wlayani Muleba 
#Bukobawadau Jan 29,2017.

Next Post Previous Post
Bukobawadau