Bukobawadau

MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NI MAZIWA BORA - WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA

waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akifurahia  ubora  wa  maziwa  ya Asas
Mkurugenzi  wa  kampuni ya  Asas Bw  Salim Abri akiteta  jambo na  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Asas  akimweleza  jambo  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  Mkuu Kasim Majaliwa akifurahi jambo na Bw Asas
Viongozi  mbali  mbali  wakimsikiliza  waziri mkuu
Waziri  Mkuu  akitoa maelezo kwa  viongozi wa  mkoa  wa Iringa
Familia  ya Asas  wakifuatilia  hotuba ya  waziri mkuu
Mkurugenzi  mtendaji  wa kampuni ya  maziwa  ya  Asas Bw  Fuad Abri akisoma  taarifa ya  kampuni  hiyo  mbele ya waziri mkuu
Wananchi wakifuatilia  hotuba ya  waziri mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi akizungumza  mbele ya  waziri mkuu
waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akifuatilia taarifa ya kampuni ya  Asas ,wengine ni salim Abri na Waziri  wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi
Farasi  waliopo shamba  la mifugo  la Asas
Askari  wa  FFU  Iringa  wakitazama ng'ombe shambani kwa  Asas
Nyati  wanaofugwa  shambani kwa Asas Iringa
Kundi  la  Nyati  wanaofugwa  shambani kwa Asas eneo la  Igingilanyi  Iringa

Askari  wa  FFU  Iringa  akipiga  picha na nyati waliopo  shambani kwa Asas
Asakari  wa FFU  Iringa  wakitazama vifaa  vya  kuhamilishia ng'ombe 
Ng'ombe  waliopo  shamba la Asas   la  Nduli
Msafara  wa  waziri  Mkuu  ukiondoka  shambani kwa  Asas
Waziri  mkuu  akishukuru kwa   wenyeji kabla ya  kuondoka
waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akiagana na  Salim  Abri
Waziri  mkuu akiagana na  mkurugenzi wa kampuni ya maziwa  ya  Asas  Fuad Abri
Waziri  mkuu  akitembelea  shamba  la mifugo  la Asas
Bw  Feisal  Abri  akimpa  maelezo  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  mkuu  akiendelea  kutembelea  shamba  la mifugo la Asas
Waziri  mkuu  Kasim Majaliwa  akitazama ng'ombe  ambao  wanasubiri  kupandikizwa mbegu
Zoezi la  kuhamilisha  ng'ombe  likifanyika
Mtaalam  akionyesha  namna ya  kupandikiza mbegu ng'ombe
Waziri  Lukuvi  kulia  akiteta  jambo na waziri  mkuu
Mtambo  wa  maziwa 
Waziri  mkuu  akifurahi majina ya ng'ombe  za  Asas
Zoezi la kukamua  maziwa  likiendelea
Waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akisalimiana na Salim Asas  baada ya  kufika  kutembelea  shamba la mifugo  katikati ni mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza
Waziri mkuu  Kasim  Majaliwa na  viongozi  mbali mbali  wakielekea  kutembelea shamba la mifugo ya  Asas( picha na MatukiodaimaBlog)

Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI  mkuu Kasim Majaliwa amepongeza  kampuni ya maziwa ya  Asas  Dairies Limited kwa  uzalishaji wa bidhaa bora  nchini  na  kuwa ni kampuni pekee  ambayo inafanya  vizuri  katika utengenezaji wa bidhaa bora za maziwa na kuwa  imeweza kutekeleza kwa  vitendo kauli  mbiu ya  Rais Dkt  John Magufuli  ya Tanzania  ya  viwanda .


Kuwa  serikali  itaendelea   kuiunga  mkono kampuni  hiyo ya  Asas  ambayo pamoja na  kufanya  vizuri katika ubora  wa  maziwa  bado   ni  kampuni yenye sifa nzuri ya  ulipaji wa  kodi nchini  pia  ni kapuni ya mfano kwa  ufugaji bora  wa ng’ombe

“ Nimefurahishwa na ufugaji  bora  ufungaji  wa  mifugo   unaofanywa na Shamba la kampuni ya Asas ya mkoani mkoani Iringa  ni  mzuri  sana lazima   wafugaji wengine nchini  kufika kujifunza jinsi ya ufugaji .”

Alisema   kuwa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya Asas Dairies kama  mtindi  unaozalishwa na kampuni hiyo ya  Asas ni mzuri  na hata  ukinywa hauna  hofu ya kuharisha kama mtindi inayotengenezwa na wengine 


Akizungumza leo  wakati wa ziara  yake ya  kutembelea  shamba la Asas lililopo eneo la Igingilanyi  katika  wilaya ya  Iringa ,waziri  mkuu  alisema  kuwa amefurahishwa na ufugaji  unaofanyika katika  eneo hilo na kutaka   watu  wengine  kuanza  kufuga mifugo badala ya  kuwa  wachungaji wa  mifugo .


Kwani  alisema tatizo kubwa ya  migogoro  kati ya  wachungaji na  wakulima inasababishwa  na baadhi ya  watu kuendesha  uchungaji  wa mifugo  badala ya  kufuga  na  hivyo  kupelekea kugombea maeneo ya kuchungia huku  wakulima   wakivamiwa na wachungaji hao .


Alisema  kwa  lengo la  kukomesha  migogoro  kati ya  wachungaji na   wakulima  anawaagiza  maofisa  mifugo  kote nchini  kuanza  kuitambua  mifugo  yote na  kuiweka alama  maalum  itakayosaidia  kutambua eneo  ambalo  mifugo  hiyo inatoka na  itakuwa ni njia ya  kukomesha wachungaji  kuhama hama 


Hivyo  alisema  ni  mhimu  sana  kwa  maofisa  Mifugo  katika Halmashauri  zote nchini  kuanza  kutoa  elimu kwa  wafugaji  ili kuondokana na  kuwa  na  mifugo mingi  isiyo bora  na  badala yake  kuachana na uchungaji  wa  mifugo  na  kujikita na ufugaji .


Alisema  kuwa  kwa  upande  wa Halmashauri  za  wilaya  zote  nchini  zinapaswa  kuwapimia  na kuwapa  hati ya umiliki  wa  ardhi  wawekezaji  wote  wakubwa  waliopo katika maeneo yao  lengo  likiwa ni  kuondokana na migogoro ya  ardhi .

TAZAMA VIDEO HAPA  CHINI 
Next Post Previous Post
Bukobawadau