Bukobawadau

DC NGARA NA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele aking'oa bangi leo katika shamba la mwananchi mkazi wa kijiji cha Kazingati kata ya Keza wilayani humo ambaye alitegemea kuvuna magunia 80 na kilo moja angeuza Sh 1700 kwa wateja kutoka nchini Burundi 
NGARA: Jeshi la polisi katika wilaya ya  Ngara mkoani Kagera, linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kazingati kata ya keza wilayani humo baada ya kumkuta anamiliki shamba la ekari mbili za bangi ambayo ni aina mojawapo ya dawa za kulevya
Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mntenjele ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya amesema mkazi huyo ni Fabian Kasigo (45) ambaye alikamatwa jana katika kijiji hicho
Kanali Mntenjele alisema mkulima huyo alipohojiwa alikiri kulima kilimo hicho tangu mwaka 2001 na kwamba  mwaka huu angevuna magunia 80 ya bangi akitarajia  kuuza kila kilo moja kwa Sh17,000 kwa wateja wake wa nchini Burundi
 Alisema kilimo cha bangi   wilayani Ngara kimeshamiri  kata zilizopo mpakani na nchi jirani za Rwanda na Burundi has kata ya Ntobeye Nyakisasa Keza na Muganza ambapo jeshi la polisi limekuwa likiwakamata na kuwafikisha mahakamani.
“Tunajitahidi kuwasiliana na wananchi wenye uzalendo raia wema kutupatia taarifa za walimaji wa zao hili, kuweza kuwakamata kwani kilimo cha bangi hakitakiwi kwa mujibu wa sheria za nchi yetu” Alisema Kanali Mntenjele.
Akitoa maelezo kwa kamati ya ulinzi na usalama kwenye shamba hilo Fabian Kasigo alisema amekuwa akiuza bangi kutoka kwa wateja mbalimbali na kuitumia kama kinga ya magonjwa kwa kutumia majani yake na kuinywa kwenye maji
Alisema kwa umri wake hawawahi kuugua na akitumia bangi huwa mwili unaimarika na kwamba tangu mwaka 2001 ametumia faida ya bangi kujiinua kiuchumi kwa kununua zaidi mashamba na mifugo
Kamati ya ulinzi na usalama katika kulifikia shamba hilo ilitumia muda wa masaa mawili kwani aliingia katikati ya pori ambako kunakaa wafugaji jamii ya wasukuma na wanyarwanda na kupata mbolea ya samadi na kustawisha zao hilo
Askari polisi walilazimika kung'oa miche ya shamba la bangi ambapo ndani ya nyumba ya mtuhumiwa kulikuwa na kilo mbili za mbegu ya zao hilo ikidaiwa kulikuwa na maandalizi ya kulima ekari tatu nyingine.
 Na Shaaban  Ndyamukama
 Pata habari mpya Za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store  BOFYA HAPA KUDOWNLOAD
Next Post Previous Post
Bukobawadau