Bukobawadau

PSPTB Wajizatiti kusimamia maadili katika Ununuzi na Ugavi

Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji  wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bw.Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa wataalamu wa Ununuzi kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya Taifa. Kulia ni Afisa Uhusiano wa  Bodi hiyo  Shamim Mdee,kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo Bw. Amani Ngonyani.

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo Bw. Amani Ngonyani  akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mkakati wa Bodi hiyo kutoa elimu ya maadili kwa wanafunzi wanasomea taaluma hiyo katika Vyuo na wale walio katika shule za Sekondari Lengo likiwa ni kujenga maadili na weledi ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda.
 Afisa Uhusiano wa Bodi hiyo Shamim Mdee (kulia) akisisitiza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) umuhimu wa kuelimisha umma kuhusu  program ya miaka mitano ya Bodi hiyo katika kutekeleza mpango mkakati wake wa miaka mitano unaolenga kuelimisha umma na wadau kuzingatia maadili ya Taaluma ya Ununuzi na Ugavi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)  leo Jijini Dar es Salaam.
           
(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
Next Post Previous Post
Bukobawadau