Bukobawadau

SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI KUTOKA CCM

SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu saba wakiwemo viongozi na wanachama wanne wa CCM ambao ni Ndg Ally Mmbaga, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, Ndg Arnold Swai, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Hai, Ndg Anastazia Innocent Malamsha, Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) na Ndg Edwin Msele, Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro vilivyosababishwa na ajali ya barabarani katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro siku ya Jumapili ya tarehe 05th Februari 2017.


Ajali hiyo ilitokea majira ya jioni ikihusisha gari ya mizigo aina ya Fuso na Toyota Hilux Surf iliyokuwa imewabeba Viongozi wa CCM waliokuwa wakitoka katika kutekeleza majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa Wilayani Rombo na kusababisha vifo vyao.


Kutokana msiba huo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Iddy Juma, familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia vifo vya Viongozi wetu.  


Wana CCM nchi nzima, tunawaombea majeruhi kupona haraka, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu.  Amina.

Imetolewa na,

 

HUMPHREY POLEPOLE

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA UENEZI

06/02/2017.

Next Post Previous Post
Bukobawadau