Bukobawadau

KWA UFUPI KANYIGO NA MACHIFU (ABAKAMA)

Muonekano wa maeneo ya Kishenge -Kanyigo ,Kiziba Mkoani Kagera
Bukobawadau Media :Nitaanzia mbali kidogo. Kiziba ilijulikana kama Bunyarwai wakati wa Mukama Bike, katika karne ya 15. Ndugu yake Bike aitwaye Nkombya alikuwa ni Mukama wa Ihangiro, wote wawili wakiwa ni watoto wa Wamara, Mukama wa Himaya ya Bunyoro-Kitara. Mtoto wa Nkombya aitwaye Kiziba alikuwa mganga wa kutibu watu. Bike, baba yake mdogo na mtawala wa Bunyarwai, alipougua sana aliagizia Kiziba aje kumtibu. Kiziba alipokuja alimtibu kweli na akaamua kukaa Bunyarwai huku akipanga mbinu za kumpindua huyo baba yake mdogo. Na kweli alimuua na kukalia kiti kama Mukama wa Bunyarwai, na jina la Bunyarwai likabadilishwa na kuwa Kiziba kuanzia wakati huo. Mukama Kiziba alizaa mtoto aitwaye Ntumwa ambaye alikuja kumrithi baba yake.
Mtu mmoja aitwaye Nyakiru, mtoto wa Mukama Igaba ll wa Bunyoro aliwasili Kiziba akiwa mwindaji na kufikia Kishenge. Alikuwa hodari wa kuua wanyama na akawa anawagawia watu nyama. Watu walimpenda sana. Alipoona anapendwa kiasi hicho akaanza kusuka mbinu za kumpindua Ntumwa. Ntumwa alikuwa amemfukuza mtoto wake aitwaye Kanyamaishwa ambaye alikuwa malformed. Nyakiru aliona afanye urafiki na Kanyamaishwa ili kwa pamoja waweze kushirikiana kumpindua Ntumwa. Nafasi waliipata wakati watu wote walipoondoka ikulu (omu kikale) kwenda kushika senene na kumuacha Mukama peke yake. Nyakiru alikwenda akamuua Ntumwa, lakini akaogopa kukaa kwenye kiti cha enzi akiogopa kululumilwa. Hivyo, badala yake, akamkalisha Kanyamaishwa kwenye kiti na kanyamaishwa akawa Mukama.


Utawala uliofuata ukawa ni wa watu wawili: Kanyamaishwa as a de jure ruler na Nyakiru as a de facto ruler. Baadaye Kanyamaishwa alikuja kuwa phased out polepole, lakini kulikuwa na michochozo ya kupunguza hasira ya Ntumwa. Michochozo hiyo imeendelea katika dynasty nzima ya Nyakiru ambaye aliitwa Kibi l. Hivyo warithi wote katika lineage ya Ntumwa ni lazima wahusishwe katika michochozo hiyo wakati Mukama wa Kiziba anatawazwa. Omwami Mutaihwa, akiwa mmojawapo katika mlolongo wa warithi katika lineage ya Ntumwa, alikuwa na jukumu la kufanya michochozo inayompa Mukama legitimacy na kuepusha hasira ya Ntumwa. Hata leo hii tungeweka Mukama mpya wa Kiziba, Omwami Amos angehusika katika michochozo hiyo.
Olwekyo inywe Abakuma mwina obusikizi bungi muno omuli Kiziba. Mara niinywe musaine kwetwa Baziba okuba nimuluga ahali Kiziba wenene.
Ninshubila washobokelwa.
Credit: Enock L. Kamuzora
Next Post Previous Post
Bukobawadau