Bukobawadau

WAZIRI DKT TIZEBA AWAONYA WENYE VIWANDA VYA CHAI KUTOWANYONYA WAKULIMA WADOGO WA CHAI


mkuu  wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza aliyemwakilisha  waziri wa wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akifungua mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini uliofanyika wilayani Mufindi
Wadau  wa  zao  la chai nchini  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu  wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza(mwenye hijabu ) aliyemwakilisha  waziri wa wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba katika  ufunguzi wa mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini leo  katika ukumbi wa TRIT Ngwazi Mufindi , kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi ya chai nchini Spika (mstaafu ) Anne Makinda ,mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi hamis Umande ,Mathias Ndengi mkurugenzi wa wakala wa chai , Nicholaus Mauya mkurugenzi wa  bodi ya  chai   kutoka kulia wa kwanza waliokaa ni mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa chai Dkt Emmanuel Simbua ,Twahili Nzalewaye mkurugenzi wa maendeleo ya mazao ya  kilimo  na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam

.......................................................................................

Na MatukiodaimaBlog ,Mufindi 


WAZIRI  wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amewaagiza  wamiliki  wa viwanda  vya  chai  nchini  kununua  chai  ya  Wakulima  wadogo kwa  kuzingatia bei  elekezi ya  serikali na sio bei wanayojipangia  wao  ya  kuwanyonya Wakulima  wadogo  wa  zao  hilo la  chai nchini .

Kuwa  serikali  imedhamilia   kuwakomboa  Wakulima  wadogo wa  zao la  chai hapa nchini kama njia ya  kukuza soko la bidhaa  zitokanazo na chai hapa nchini ya  duniani ,hivyo  njia  pekee ni  kuona Wakulima  wadogo  wanaendelea  kuhamasika  kuongeza kasi ya  kilimo  hicho  cha  chai  ili  kuviwezesha  viwanda vya  chai  nchini  kuzalisha chai kwa  wingi na ubora  zaidi.

Alisema  kuwa zao la  chai ni moja kati ya mazao  yanayopelewa  kipaumbele kama mazao ya  biashara hapa  nchini na  kuwa zao  la  chai  pekee  huliingizia Taifa  wastani  wa  dola  za kimarekani milioni 50  na  kutoa ajira kwa watu  milioni 2 kwa mwaka hivyo ni zao lina lina fursa  kubwa ya  kuongeza wigo  wa kiuchumi nchini pamoja na kuendeleza  kilimo cha  zao  hilo.

Waziri Dkt Tizeba  aliyewakilishwa na mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  katika  ufunguzi huo wa mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini  uliofanyika katika  ukumbi wa taasisi ya utafiti wa chai (TRIT) Gwazi  Mufindi leo alisema  kuwa uzalishaji wa chai nchini kwa upande wa majani makavu ni wastani  wa  tani 35 kwa  mwaka wakati kwa  wakulima  wadogo  wanazalisha wanazalisha  kilo 1000 kwa hekta  kwa mwaka na  Wakulima wakubwa ni wastani wa kilo  2000 za majani makavu kwa hekta kwa mwaka  ukilinganisha takwimu  za nchi ya Kenya  ambayo tija  ni kwa  mkulima  mdogo ni wastani wa kilo 2500 kwa hekta  takwimu  ambazo zinaonyesha   sekta  ndogo ya  chai  nchini ipo nyuma  ukilinganisha na Kenya.

“Ukuaji  wa  sekta  ndogo ya  chai  Tanzania ni mdogo  sana  ukilinganisha na nchi  kama Rwanda na Uganda ila  kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza uzalishaji wa tija ya  chai ya  Tanzania  kwa  kuwa nia ya  kuendeleza  zao la chain a ardhi  ipo ….naomba  kutoa rai  kwenu  wadau kuweka mipango ya  kuendeleza  kilimo hiki na serikali ipo nyuma yenu “

Alisema kuwa serikali  imedhamilia  kushirikiana na wadau wa  chai kwa kuongeza ardhi  kwa maeneo yanayolima  chai hadi kufikia hekta  27000 kuwa mwaka 2021/2022 hekta  kutoka  22721 kwa  sasa  pia  kuongeza uzalishwaji wa chai  kavu kutoka wastani wa tani 32 kwa mwaka hadi kufikia  zaidi ya tani 50,000 mwaka  2021/2022 na  kuongeza uzalishaji wa tija kutoka  kilo  1000 kwa mwaka hadi  zaidi ya  kilo 2000 za majani makavu.

Awali mwenyekiti wa mkutano huo spika  wa  bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania (mstaafu)  Anne Makinda ambae ni mwenyekiti wa boi ya chai nchini  alisema  kuwa kero  kubwa ya  Wakulima  wadogo wa chai ni mbolea kwa ajili ya kukuzia zao  hilo kwani  zao  hilo Wakulima hawana  ruzuku ya serikali Kuwa  mbolea  inayotumika kwa zao la chai ni tofauti na ile ya mazao ya mahindi japo  changamoto hiyo wanaendelea  kuijadilia pamoja na  serikali  huku  akidai kuwa  chai ya Tanzania  inauzwa kwa bei ndogo  sana  kutokana na ubora  wake kuwa duni  ukilinganishwa na chai ya Wakulima  wadogo wa Rwanda ambao  walikuwa katika vita leo  wamefikia  chai kavu zaidi ta tani 20,000 lakini Tanzania  ambayo ilipata  uhuru miaka  50  iliyopita  chai haina ubora

“ Yawezekana  wenzetu kwa  kuwa ni Wakulima  wapya  wanatumia  vikonyo vipya na maeneo mapya ndio maana  wanatuzidi ila  sisi  bado  tunatumia  vikonyo vya  zamani na ardhi  iliyochoka “

Makinda  alisema migogoro  midogo midogo inayoanzishwa na viongozi  katika maeneo ya  Wakulima wa chai  ni changamoto ya kurudisha  nyuma kasi ya  uzalishaji wa  zao la  chai nchini hivyo  zinahitajika  jitihada za  kuondoa migogoro  hiyo ili  kukuza zao la chai nchini
MWISHO 

Next Post Previous Post
Bukobawadau