Bukobawadau

WILAYANI NGARA:RISASI ZAOKOTWA ZIKIWA ZIMETELEKEZWA

 Askari polisi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera akishuhudia  Risasi 193 za silaha mbalimbali zinazotumika kuuwa wanyama kwenye hifadhi baada ya kuokotwa kandokando ya mto Ruvubu katika daraja kuu la Kasharazi kutoka mjini Ngara kuelekea Benaco wilayani, leo April 19,2017 saa 10 alasiri
Wananchi wa kijiji cha Kasharazi wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakichunguza Risasi 193 zilizookotwa  leo April 19, 2017  baada ya kutelekezwa  na watu wasiojulikana kando ya daraja la mto Ruvubu barabara kuu ya Ngara hadi eneo la K9 katika kijiji hicho.
Askari polisi wa wilaya ya Ngara makao makuu ya polisi ya wilaya mkoani Kagera wakishuhudia  Risasi 193 za silaha mbalimbali zinazotumika kuuwa wanyama kwenye hifadhi baada ya kuokotwa kandokando ya mto Ruvubu katika daraja kuu la Kasharazi kutoka mjini Ngara kuelekea Benaco wilayani Ngara leo saa 10 alasiri
 Muonekano wa Risasi zikiwa zimetapakaa kando kando ya daraja la  Kasharazi zilizookotwa na wananchi leo April 19,2017
Askari polisi wa  Wilaya ya  Ngara mkoa wa Kagera  PC Samweli Shayo (kushoto)na  PC Slivanus (kulia) wakichunguza Risasi 193 zilizookotwa na wananchi wa kijiji cha Kasharazi wilayani humo jana April 19, 2017  (leo) baada ya kutelekezwa  na watu wasiojulikana kando ya daraja la mto Ruvubu barabara kuu ya Ngara .

Picha na Shaaban Ndyamukama

Next Post Previous Post
Bukobawadau