Bukobawadau

MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE.

Pichani Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba, Mh. Murshidi Hashim Ngeze, akizungumza na hadhala iliyohudhuria Mkutano wake Katani Rubale
 Bi Asuma Kokugonza Bantanuka, (Diwani viti maalum Tarafa Ruabale - CCM) Akizungumza na wananchi waliohudhuria Mkutanoni.

Na Dulla, Kasibante Fm.
Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Ipo katika Mkakati na Hatua za Awali za kuyapeleka Makao Makuu ya Wilaya Bukoba, katika tarafa ya Rubale, Kata Rubale.
Hayo yamebainika katika Mkutano wa Hadhala wa Wananchi pamoja na wadau wa Elimu, uliofanyika katika Kata ya Rubale Juni 3, 2017.

Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Mh. Murshidi Hashim Ngeze amesema, tayari Halmashauri imekwishatuma timu ya Wataalamu kukagua maeneo wapi panafaa kuwekwa Makao Makuu hayo ya Wilaya, Rubale ikiwa ni eneo mojawapo linalopewa kipaumbele, hivyo wananchi wawe tayari kuyapokea maamuzi hayo pale yatakapopitishwa.
 Pichani Afsa mtenndaji wa Kata Rubale Bwn, Abdallah Rwabigimbo

Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Mwenyekiti Ngeze amesema kuwa tayari mazungumzo ya awali yameanza kufanyika ikiwa ni pamoja na kuanza mipango ya kuanza kuifanya Rubale kuwa Mji mdogo, huku akitoa Rai kwa Wananchi kukubali usumbufu na uharibifu utakaojitokeza kuhusiana na mali zao, kwani Maendeleo pia huambatana na hasara.

Awali mwenyekiti Ngeze ambae pia ni Diwani wa Kata ya Rukoma, amewapongeza wananchi kwa kujitolea kuchangia vifaa vya ujenzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Rubale, na kuahidi kuendelea kutafuta wahisani mbalimbali ili kuchangia Ujenzi wa Shule hiyo, na kusisitiza kuwa Shule hiyo ambayo inapendekezwa kuwa ya Wasichana pekee ni lazima itajengwa Rubale.

Kwa upande wake Diwani wa viti maalumu Tarafa Rubale kupitia CCM, Bi Asuma Kokugonza Bantanuka amewaomba akina mama kujitokeza kwa wingi kuunga mkono Ujenzi huo, na kuwataka wnawake ikibidi kujitoa na kujitolea kufanikisha zoezi hilo, lengo likiwa ni kumsomesha mtoto wa kike kwa maendeleo ya Baadae. 
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria Mkutano huo, wakiendelea kufuatilia hotuba.
 Alhaji Amri Rashidi Kilahama, kutoka Kabirizi akifuatilia jambo katika mkutano
 Bwana Rwechungura Iddy akichangia jambo
 Walimu kutoka chuo cha Frances International College nao walikuwepo.
 Miongoni mwa wazee waliowakilisha wananchi kutoa yao ya moyoni ni pamoja na Mzee Sadick kama anavyoonekana pichani..
 Mwenyekiti akionekana kuridhishwa na nguvu ya wananchi ya michango yao ya Vifaa  vya Ujenzi wa Kidato cha tano na sita.
 Mwenyekiti akionekana kuridhishwa na nguvu ya wananchi ya michango yao ya Vifaa  vya Ujenzi wa Kidato cha tano na sita.
 (Picha zote na Allawi Kaboyo)
Next Post Previous Post
Bukobawadau