Bukobawadau

OFISI YA WAZIRI MKUU YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiongea na  wafanyakazi wa ofisi hiyo (hawako pichani) wakati wa mkutano wa kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma uliofanyika    leo jijini Dar es salaam tarehe 23 Juni, 2017
 Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano wa Kuadhinmisha wiki ya utumishi wa umma uliofanyika    leo jijini Dar es salaam tarehe 23 Juni, 2017.

Ofisi ya Waziri Mkuu
imeadhimisha
wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia Juni 16-23 Barani Afrika,  kwa mwaka huu kauli mbiu  ni “Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utoaji Huduma: Vijana washirikishwe kuleta Mabadiliko Barani Afrika”.
Kwa kuzingatia kauli mbiu hiyo yenye kujikita katika kushirikisha jamii katika utoaji huduma, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua amekutana na wafanyakazi wa ofisi hiyo leo jijini Dar es salaam tarehe 23 Juni, 2017,   ambapo wamejadili jinsi ya kuboresha utoaji wa huduma kwa umma kwa kuzingatia weledi, uadilifu na ufanisi ili kuhakikisha Dira na Dhima ya Ofisi hiyo inafikiwa.
Dira ya Ofisi hiyo ni kutoa huduma kwa umma katika mazingira shindani ya kiuchumi ili kuwa na maendeleo emdelevu, aidha Dhima ya ofisi hiyo ni Kuratibu na kusimamia utoaji wa huduma zenye kuleta matokeo yanaotarajiwa katika sekta zote ili kujenga mazingira ya kiuchumi kwa maendeleo enndelevu.Ofisi ya Waziri imekuwepo tangu mwaka 1962. Mwaka 1977, Ofisi ilipewa hadhi yake kisheria kwa kuzingatia Katiba ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ilianzisha wadhifa wa Waziri mkuu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau