Bukobawadau

KAIRUKI HOSPITALI YAZINDUA KITENGO CHA KUCHUJA DAMU KWA WAGONJWA WENYE MATATIZO YA FIGO

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijjini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki, Kokushubila Kairuki.
Mkurugenzi Mkuu wa Kairuki Hospitali Dk. Asser Mchomvu, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki akitoa hotuba yake.
Dk.Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda.
 Dk.Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akipata maelezo alipotembelea kitengo cha kuchuja damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.
Baadhi ya madaktari waliohudhuria hafla hiyo wakisikiliza hotuba za viongozi. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu, Eva Beatus.
 Jengo la Kitengo hicho.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, akitoa hotuba yake.
SPIKA Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya( NHIF), Anne Makinda,amewataka watanzania kutumia Mfuko wa Taifa wa Bima hiyo ili kupata unafuu wa matibabu pindi wanapougua.
Wito huo alitoa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti huyo wakati alipozindua kitengo cha kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Kairuki.
Alisema, kutokana na gharama ya matibabu kupanda kila siku,kadi za bima ya afya zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupata unafuu wa matibabu kipindi mgonjwa anapokuwa hana fedha.
Makinda, alisema bima hiyo inatoa fursa kwa wanachama kupata huduma za matibabu katika hospitali wanazoona zinatoa huduma nzuri na kumjali mgonjwa.
“Vituo vyenye huduma ya NHIF vinapaswa kutibia wagonjwa kwa kuwajali , kuwapenda pamoja na kuwa wakarimu kwa wagonjwa kwani huduma hii inasaidia sana watu hasa wale wanaougua magonjwa yenye kulipia gharama kubwa,”alisema Makinda.




Next Post Previous Post
Bukobawadau