Bukobawadau

KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), akizungumza na uongozi wa wilaya ya Kakonko, alipokuwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), akikagua kalvati  katika barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (aliyevaa suti) akikagua matofali katika kambi ya mkandarasi ya Nyanza Road Works alipokuwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma

Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inaojengwa kwa kiwango cha lami. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.

Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura (kulia), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), aina ya kokoto zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), akisisitiza jambo kwa Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura (kushoto), wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.

Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami  Dunaka Screenivasa Rao akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi huo mkoani Kigoma.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Next Post Previous Post
Bukobawadau