Bukobawadau

KATIKA PICHA SHUGHULI YA MATANGA YA BI ANASTAZIA RWECHUNGURA WA KIJIJINI GERA

 Familia ya Marehemu Mzee Gervas Rwechungura wameweza kuungana na jamaa na marafiki katika shughuli ya kuanua matanga ya mpendwa mama yao mzazi Bi Anastazia Gervas Rwechungura kufuatia kifo chake kilichotokea Des26,2017 na mazishi yake yalifanyika Jan5,2018.Na Shughuli hii ya matanga iliyofanyika juma lililopita nyumbani kwao Kijijini Kashambya Gera.
 Sehemu ya waumini wakishiriki Ibada ya Matanga ya Bi Anastazia Rwechungura aliyefarika tarehe 26.12.2017Shughuli ya Ibada ikiwa inaendelea
 Wanafamilia wakiendelea kushiriki Ibada hiyo, hakika Mama yetu Bi Anastazia atakumbukwa daima kwa mambo mengi aliyoyafanya kwa umahiri mkubwa katika harakati za maendelea na kama mhasisi wa TANU na kiongozi wa UWT Kitaifa
Hivi ndivyo wadau walivyojitokeza kushiriki shughuli ya matanga ya mpendwa wetu mwanaharakati wa maendeleo kitaifa na kimkoa Bi Anastazia Rwechungura
Ibada ikiendelea
Ni wakati wa kutoa sadaka kwa watu wote wakiongozwa na wanafamilia
Wanafamilia wakiendelea kutoa Sadaka 
Wajukuu wakielekea kutoa sadaka kwa ajili ya kumuombea bibi yao Mpendwa
Mwendelezo wa matukio wakati zoezi la kutoa sadaka likiendelea
Mh. Diwani wa Gera Mzee Bitegeko akitoa sadaka yake, Ikumbukwe Mh. Bitegeko mapema mara baada ya taarifa za msiba huo akieleza wasifu wa Bi Anastazia alisema ;'Ma Anastazia Grevace Rwechungula wa Kashambya Gera, amefariki tarehe 26/12/2017 mazishi ni tarehe 05/01/2018 saa 4.00 asb hadi saa 11.00 alasiri. Huyu mama Shupavu ni Mhasisi wa TANU na CCM, aidha aliwahi kuwa kamanda wa TYL kitaifa, kamanda wa Scout Kitaifa, kiongozi wa UWT Kitaifa. Mshauri na Mdau wa Maendeleo Mkoa, Wilaya na Kata yetu Gera. Mambo mengi ya kimaendeleo wametufanyia, pomoja na kuchimba maji kwa wananchi. Kwa sasa kumuenzi Binti yake Conso anajenga Hospital Kubwa hapa Gera, ipo hatua za mwisho, na vifaa vyote vimeishafika'. Mwisho kabisa alimaliza kwa kuwaomba wakazi wa Gera watambue  mchango wake na penye uwezekano waungane kumsindikiza  apumzike Salaama. Bwana alitoa Bwana ametwa Jina lake Lihimidiwe. Amin
Utaratibu wa kutoa Sadaka ukiendelea
Paul Rwechungura ,Conso Rwechungra na Peter Rwechungura wakiendelea na Ibada ya kumaliza matanga ya mama yao mpendwa Bi Anastazia Rwechungura
Neno la bwana likisomwa mwanzoni kabisa mwa Ibada.
 Taswira umati ukiendelea kushiriki Ibada.
Ndugu jamaa marafiki na majirani wakiendelea kushiriki Ibada maalumu kumaliza matanga ya mpendwa wao Bi Anastazia Gervas Ishengoma shughuli iliyofanyika nyumbani kwake kijijini Gera.
 Fr. wa Parokia ya Gera akiongoza Ibada maalumu ya kumaliza matanga msiba Bi Anastazia Rwechungura




Waumini wakiendelea kupata Komonio katika Ibada ya matanga msiba wa Bi Anastazia Rwechungura




Waumini wakiendelea kupata Komonio katika Ibada ya matanga msiba wa Bi Anastazia Rwechungura
Bwana Thomas Charles (Katikilo)na Kijana Alex marafiki wa familia.
 Waumini wakiendelea kushiriki Ibada
 Waumini wakipeana mkono wa amani mara baada ya Ibada kukamilika






 Dada Conso(Dkt. Merry ) akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia


bukobawadau tunatoa pole sana kwa wanafamilia kwa msiba huu mzito,tupo pamoja katika sala na Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi kigumu cha majonzi. ... Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mama yetu mpendwa mahali pema peponi.Amen!!
 Padre akinyunyizia maji ya baraka kwenye kaburi ya mpendwa wetu Bi Anastazia Rwechungura.






Ibada maalumu eneo la kaburi alipo pumzika Bi Anastazia Rwechungra


bukobawadau tunatoa pole sana kwa wanafamilia kwa msiba huu mzito,tupo pamoja katika sala na Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi kigumu cha majonzi. ... Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mama yetu mpendwa mahali pema peponi.Amen!!




Mama mkali wa mapishi pichani wakuitwa Mama Achi
Muendelezo wa matukio ya picha
Kijana mpambanaji Alex pichani


 Wananchi wakiendelea kufurahia kinywaji kwa pamoja
 Ndugu wakipata huduma ya Chakula mara baada ya Ibada kukamilika.
Wananchi marafiki wa familia ya Marehemu mzee Gervas Rwechungura wakipata chakula cha mchana baada ya kukamilisha Ibada maalumu ya kumaliza matanga ya Mpendwa wao Bi Anastazia Rwechungura.


Huduma safi ya msosi ikiwa inaendelea kutolewa kwa watu






Wadau katika picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu.




Bi Mainda Kassim wakati akiwasili kuungana na familia ya Rwechungura katika shughuli ya matanga.
Vyama vya wanawake wakiwajibika kwa kusaidia kuchota maji
 Wadau wakishow love mbele ya Camera yetu moja kwa moja kutoka Kijijini Kashambya Gera
Taswira eneo la tukio shughuli ya kumaliza matanga ya Bi Anastazia Rwechungura
Bwana Soma akipokea kinywaji mjalabu kabisa...!


Wadau wakicheck na camera yetu.
Huduma ya vinywaji ikiendelea kutolewa


Mpaka kufikia mwisho ilikuwa ni mwendo wa Kula kunywa na furahi kama unavyoweza kujionea kupitia picha
Mwisho bukobawadau tunatoa pole sana kwa wanafamilia kwa msiba huu mzito,tupo pamoja katika sala na Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi kigumu cha majonzi. ... Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mama yetu mpendwa mahali pema peponi.Amen!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau