Bukobawadau

MAZISHI YA MZEE PETRO JOSEPH MUTALEMWA YALIYOFANYIKA KIJIJINI KIBENGEWE-BUKOBA

Ni simanzi na huzini mkubwa kwa familia ya Marehemu mzee Petro Joseph Mutalemwa aliyezaliwa mnamo tarehe 24.10.1922  na kufariki Jan 6,2018 akiwa na umri wa miaka 96.
Shughuli ya mazishi ya mpendwa Mzee Petro J. Mutalemwa aliyewahi kuwa Daktari katika hospitali ya Taifa Muhimbili na hospitali ya Mkoa Kagera na Bugando Jijini Mwanza imefanyika siku ya Jumanne Jan9,2018 nyumbani kwake Kijijini Rushaka-Kibengwe Bukoba Vijijini na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji
Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu, mzee wetu Dkt. Petro Mutalemwa aliyepata elimu yake ya sekondari katika seminari ya Rubya na Katigondo.
Msemaji wa familia akitoa Utaratibu muda mchache kabla ya kuanza kwa Ibada maalumu.
Wajukuu wakiwa wamebeba msabala wakati mwili ukitolewa ndani.
Sehemu ya kuweka Jeneza lenye mwili ya mzee wetu Petro Mutalemwa aliyewahi kufanya kazi katika Jeshi la Polisi la mkoloni wa Kiingereza wakati wa uhai wake
Marehemu mzee Petro Joseph Mutalemwa pichani enzi za uhai wake,Marehemu alipata kujiunga na mafunzo ya maabara mwaka 1949 na kuajiliwa katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es Salaam na kisha kufanya kazi katika hospital ya Bukoba na hospitali ya taifa ya muhimbili.
Wakati Jeneza likiwa linatolewa ndani kwa ajili ya Ibada maalumu,Tunamuomba Mungu aipokee roho ya marehemu na ampumzishe kwa amani
Sehemu ya wajukuu na wanafamilia wakiwa tayari kushiri Ibada hiyo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu  Kijijini Rushaka-Kibengwe 
Watawa wa Kikatoliki wakiwa tayari kushiriki Ibada maalumu ya kumsindikiza mpendwa mzee Petro Joseph Mutalemwa wa  Kijijini Rushaka-Kibengwe Bukoba Vijijini
Umati wa waombolezaji wakati wa Ibada ya kumsindikiza mzee weto mpendwa daktari Petro Joseph Mutalemwa (96).
 Mapadre wapatao 13 wameweza kushiriki Ibada hiyo Msgr.Gozibert, Fr. Pholbart. Fr. Samuel,Fe.Cornel,Fr.Switbert,Fr.Delphinius,Fr. Deodatus,Fr. Prosper,Fr Johannes, Fr.Christopher,Fr.Edwin pamoja na Fr. Jason waki wameungana na familia ya mpendwa wetu Mzee Petro Joseph Mutalemwa  katika shughuli ya mazishi iliyofanyikaKijijini Rushaka-Kibengwe  Jan9,2018.
Taswira eneo la tukio Shughuli ya Ibada ikiwa inaendelea
Waomnolezaji wakiendelea kushiriki Ibada hiyo
Mapadre wakiongozwa na Msgr Gozibert 
Fr. akitoa shukrani kwa watu wote walioshiriki shughuli ya mazishi ya Mjomba wake
Marehemu Mzee Petro ameacha mjane na watoto 8 ambao ni Costantin Mutalemwa, Salvatory Mutalemwa hawapo pichani wengine ni Rosebekta Mutalemwa,Winifrida Mutakemwa,Angela Mutalemwa,Wence Mutalemwa,Grace Mutalemwa na Liberatus Mutalemwa.
Kupata Komonio wa Wakatoliki walioamini
Endelea kuwa nasi mpaka mwisho kwa mtiriko mzima wa matukio ya picha
Bukobawadau tunatoa pole sana kwa wanafamilia kwa msiba huu mzito,tupo pamoja katika sala na Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi kigumu cha majonzi. ... Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mama yetu mpendwa mahali pema peponi.Amen!!



 Adv. Kabunga mwakilishi wa Chama cha mawakili wa Kanda ya Ziwa
Salaam za rambirambi kutoka kwa Jijijini Mwanza
Mwenyekiti wa Kijiji akitoa salaam za rambirambi.
 Bi Winnie Mtalemwa mtoto wa kuzaliwa na marehemu mzee Petro Mutalemwa
Rambirambi kutoka kwa mtoto wa Ubatizo


Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika shughuli ya mazishi ya mpendwa wetu mzee Petro Mutalemwa
Wakati wa kutoa heshima za mwisho 
 Mama Kyaruzi mwanaukoo wa familia hii akitoa heshima zake za mwisho kumuaga mpendwa mzee Petro Joseph Mutalemwa.






 Wanakwaya wa JohnBosco wakati wa Ibada ya maziko ya mpendwa mzee Petro Mutalemwa
Wakati zoezi la kutoa heshima za mwisho ukiwa unaendelea
 Wanafamilia machozi yakiwatoka wakati wa kutoa heshima za mwisho kumuaga mpendwa.
Zoezi la kutoa heshima za mwisho likiendelea
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri msibani hapo.
Wanakwaya wakitoa heshima za mwisho kumuaga mpendwa Mzee Petro Mutalemwa
#BUKOBAWADAUMEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045/0754 505043
Poleni sana wafiwa.
Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu mzee Petro Mutalemwa likiingizwa kaburini
Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya mwisho ya Mpendwa wetu Mzee Petro Joseph Mutalemwa.


Padre akiweka Udongo kwenye kaburi
Simanzi kubwa kwa wanafamilia wote
Utaratibu wa kuweka udongo kwenye kabri pichani anaonekana Fr.Philbert baroko wa Kibengwe akiwa tayari kuweka Udongo
Mjane wa marehemu akiweka Udongo kwenye kaburo
Wafiwa na Makundi mbalimbali wakiwa mashada yao mkononi


Kwa pamoja wakiweka mashada ya maua
Bi Winifrida Mutalemwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa baba yake
Bi Winifrida Mutalemwa mara baada ya kuweka shada la maua
Muonekano wa nyumba ya Milele ya mpendwa wetu Mzee Petro Joseph Mutalemwa


Utayari wa kuweka mashada kwenye kaburi la mpendwa wetu Mzee Petro Mutalemwa

Muendelezo wa matukio ya picha eneo la kaburi
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri msibani hapo.
 Wajukuu katika picha ya pamoja na Bibi yao Mjane Ma Costantina Mutalemwa
Wajukuu katika picha ya pamoja na Bibi yao Mjane Ma Costantina Mutalemwa


Huduma safi ya msosi ikiendelea kwa watu wote.
Wadau wakiendelea kupata msosi
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri msibani hapo.
Wajukuu wakipata msosi safi ulioandaliwa
Taswira msibani hapo wakati zoezi la kupata chakula likiendelea
Waombolezaji wakiendelea kupata huduma safi ya chakula kilichoandaliwa
Baadhi ya waombolezaji wakibadilishana mawazo.

Mungu aipokee roho ya marehemu na ampumzishe kwa amani
#BUKOBAWADAUMEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045/0754 505043
Mwisho Bukobawadau tunatoa pole sana kwa wanafamilia kwa msiba huu mzito,tupo pamoja katika sala na Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi kigumu cha majonzi. ... Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mama yetu mpendwa mahali pema peponi.Amen!!




Next Post Previous Post
Bukobawadau