SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

20 January 2018

NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI ZINAVYOIHANGAISHA WILAYA YA MISSENYI

 Mkuu wa Wilaya  Missenyi Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera Luteni kanali Denis Mwila akihutubia katika uzinduzi wa kampeni
 Missenyi,
Jumla ya kesi 31 zimepokelewa na jeshi la polisi wilayani missenyi mkoani kagera  zikihusisha makosa ya mimba pamoja na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa mwaka 2017
Hayo yamebainishwa na koplo RASHID RAMADHAN afisa wa polisi dawati la jinsia wilayani missenyi alipokuwa akitoa taarifa ya jeshi la polisi wilayani hapa katika uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ndoa za utotoni inayoendeshwa na shirika la World Vision Tanzania
Amesema kuwa kati ya kesi hizo,20 zimeshakamilishwa ushahidhi ka kufikishwa mahakamani,7 watuhumiwa bado wanaendelea kutafutwa na 4 ziko chini ya upelelezi wa jeshi hilo.
Naye afisa ustawi wa jamii wilayani missenyi ANORD NKONGOKI amesema kuwa kwa mwaka 2017 walipokea jumla ya malalamiko 31 yakihusisha  wanafunzi kupatiwa ujauzito ambapo baada ya kuzipokea walilazimika kulishirikisha jeshi la polisi ili kuwatafuta wahalifu na baadhi ya kesi hizo zimekwishafikishwa mahakamani.
Bwana NKONGOKI ameongeza kwa kuzitaja baadhi ya sababu zinazopelekea ndoa pamoja na mimba za utotoni kuwa ni umaskini 
wa kipato kwa wazazi ambapo hulazimika kuwaoza watoto ili wapate mali,tama kwa watoto wa kiike pale wanaporubuniwa na vijana hasa kundi la boda boda sanjari na wazazi kutengana na kupelekea kutowajali watoto
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya missenyi kanali DENICE MWILA amesema kuwa maendeleo ya nchi yamekuwa yakirudishwa nyuma kutokana na wimbi wa mimba za utotoni ambapo watoto hujikuta wakipoteza malengo yao na kusema kuwa serikali wilayani hapa inaendelea na mpango wa kudhibiti janga hilo kwa kuendelea 
na msako kwa vijana wanaojihusisha na vitendo vya kimahusiano pamoja na wanafunzi

Aidha mratibu wa shirika la World Vision Tanzania mkoani Kagera ambalo ndilo linaratibu kampenin hiyo, bwana RENATUS RUGAKINGILA amesema kuwa shirika hilo limeamua kuanzisha kampeni hiyo kufuatia watoto wengi hasa wa kike kupoteza ndoto zao kutokana na janga la ndoa za utotoni na kuongeza kuwa watatoa elimu kwa jamii kila sehemu hasa katika mikutano ya vijiji na mashuleni ili jamii ipate uelewa wa kutosha juu ya athati zinazotokana na ndoa za utotoni.
NA AVITUS MUTAYOBA

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU