SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

21 January 2018

PICHA YETU YA LEO KATIKA HISTORIA

 Jengo la Nyalulembo Center lililopo katika kata ya Gera Kijiji Kashambya  tarafa Kiziba Wilayani Missenyi eneo maarufu kama kwa (mkama/mfalme Lutinwa)historia ya Buhaya inaonyesha eneo hili lilitawaliwa Nyakiiru (Kibi) mmoja wa watoto wa Nyunaki mmoja wapo kati ya wake wengi wa Igaba.
Bwana Stuhimann ameandika katika kitabu chake kiitwacho ''Milt Emin Pasha ins Hers Von Afrika''ukrasa wa 138 habari ya kupendeza isemayo;'Kiziba tangu mwanzo ilijenga na sehemu nyingine za Buhaya ni sehemu pekee ambayo watawala wake wanahusiana kidogo na wenyeji wa asili,ujirani wa Buganda uliwezesha Elimu na Ustaarabu wao kuenea zaidi kuliko mahali pengine,kukaa mpakani na kujishughulisha na biashara ya pembe ya za ndovu kuliwatia moyo wenyeji mpaka kipindi wanakutana na Waarabu.Wenyeji wa Kiziba ni wasafiri sana na hii ni kwa sababu waliweza kujifunza lugha na elimu mpya za wageni katika ardhi yao wenyewe ni rahisi kwao kuacha mila zao za zamani katika harakati za kimaisha kuliko majirani wao wengine na maeeo ya  kusini.
Masimulizi ya kale yanaonyesha Nyakiiru na Ruhinda aliyemiliki Karager walikuwa ndugu .Kiziba ni falme kati ya falme saba zinazojenga jamii kubwa ambayo kwa sasa inajulikana kama Buhaya.Historia ya miaka mia tano iliyopita inaonesha tayari falme hii ilikuwa himaya iliyokuwa tayari imejikita kwenye eneo ambalo kwa sasa linajulikana kama tarafa kiziba.Kwa sasa tarafa kiziba ni eneo la kiutawala ambalo ni tarafa yenye kata kumi kati ya kata za wilaya Missenyi.Kata hizo ni kashenye,kanyigo, Bwanjai,Buyango, Ruzinga,Kitobo, Bugandika Gera,Ishozi na Ishunju
#Bukobawadau21Jan2018

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU