SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

20 January 2018

WAATHIRIKA WA MABOMU WAZIDI KUSAIDIWA

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luten Kanali Michael Mntenjele (kushoto) akipokea taarifa ya madawa na vifaa tiba kutoka kwa mfamasia wa halmashauri ya wilaya hiyo Patrick Ogo (mwenye koti jeusi katikati) vyenye thamani ya Sh 11.34 milioni baada ya kuwasilishwa leo katika Hospitali ya misheni Rulenge na afisa Mahusiano wa Kampuni ya Kabanga Nickel Francis Wikdez (Kulia)
Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Kabanga Nickel wilaya ya Ngara mkoani Kagera Francis Widkez (Kushoto) akimkabidhi vyakula vya waathirika wa bomu diwani wa kata ya Kibogora Adronis Bulindoli ili akabikabidhi wa wahanga ambao waliopoteza wanafunzi watano katika tukio la Novemba mwaka jana kama mkono wa pole ambapo kampuni hiyo imetoa msaada wa sare vyakula vifaa vya shule na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh20.3 milioni
Picha na habari kwa hisani ya Shaaban Ndyamukama
 Wahanga wa bomu la kutupwa kwa mkono lililowalipukia wanafunzi wa darasa la kwanza  katika shule ya msingi Kihinga wilaya ya Ngara mkoani Kagera Novemba  mwaka jana wamepata msaada wa vitu mbalimbali kukidhi maisha yao
Katika tukio hilo  lililosababisha vifo vya wanafunzi watano wa darasa  kwanza na majeruhi 43 ambao baada ya kuruhusiwa toka hospitali ya Rulenge wameendelea kupata msaada  kutoka kwa wafadhili mbalimbali
Kampuni ya Kabanga Nickel iliyoko wilaya ya Ngara mkoani Ngara imetoa msaada wa sare, vifaa vya kufundishia na kujifunzia ,vyakula , dawa  na vifaa tiba kwa wahanga hao vyenye thamani ya Sh20.32 milioni  kwa wanafunzi 192 ambao sasa wameingia darasa la pili katika shule hiyo

Afisa mahusiano ya kampuni hiyo Francis Wikdez akikabidhi vifaa hivyo kwa wazazi walimu na uongozi wa serikali ya wilaya ya Ngara shuleni hapo juzi  alisema sare za shule kwa wanafunzi hao  vikiwemo vifaa vya shule  gharama yake ni  Sh8.7 milioni  
Wikdez alisema pia kampuni hiyo ilitoa msaada wa dawa na vifaa tiba katika hospitali ya Rulenge vyenye thamani ya Sh11.34 milioni   kufidia matumizi ya dawa  na vifaa hivyo wakati wa kuhudumia majeruhi 43 waliojeruhiwa na bomu katika tukuo hilo ili kuendelea kuhudumia wagonjwa wanaoletwa hospitalini hapo.
Alisema katika vyakula vilivyotolewa na kampuni hiyo ni kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa familia tano zilizopoteza watoto wakati wa tukio la bomu na   kila familia ilipatiwa kilo tano tano za Mchele, Mahindi maharage na sukari pamoja na lita nne za mafuta ya kupikia.
 “Sisi kama sehemu ya jamii tunaungana na wanajamii wengine kutoa msaada huu kuwafariji watoto na wazazi wao lakini kuwatia moyo wa kuendelea na masomo wakijengeka kisaikolojia kusahau tukio lililotokea”Alisema Wikdez
Naye diwani wa kata ya Kibogora ilipo shule ya msingi Kihinga Adronis Bulindoli, alisema hali ya mahudhurio ya wanafunzi inaridhisha ikiwa ni pamoja na wazazi kuendelea kuandikisha watoto wanaoanza darasa la kwanza na elimu ya awali licha ya kuwepo changamoto za miundombinu ya kufundishia.
Bulindoli alisema kufikia januari 16 mwaka huu wameandikishwa wanafunzi wa elimu ya awali  126 kati ya 200 waliotegemewa na darasa la kwanza wameandikishwa 232 kati ya 296 waliofanyiwa maoteo
Pia  mkuu wa wilaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya  hiyo alisema hali ya   usalama imeimarika baada ya  wataalamu wa milipuko ya mabomu kufika kwenye   shule hiyo na kufanya uchunguzi wa kimazingira na kutoa taarifa kwamba  hakuna madhara dalili htarishi za usalama
 “Tunazidi kusisitiza  hairuhusiwi tena kufanyika kwa biashara ya vyuma chakavu ambavyo ndivyo vilikuwa chanzo cha tukio hilo na wanafunzi  wetu kuathirika” Alisema Kanali Mntenjele
Katika hatua nyingine   aliwataka walimu kuwasajili wanafunzi wanaoletwa na wazazi bila  kuka kamilisha sare ili waanze masomo na wazazi wahakikishe wanatoa mahitaji ya watoto wao kufikia mwezi Machi mwaka huu. 
 Mganga mkuu wa hospitali ya Rulenge Wilayani Ngara Sista Mariagoleth Fredrick akipokea dawa na Vifaa tiba vilivyotolewa juzi na kampni ya Kabanga Nickel kufidia vifaa vivyotumika kutib wanafunzi majeruhi wa mabomu katika shule ya Msingi Kiginga Wilayani humo Novemba mwaka jana
Ngara: Na Shaaban Ndyamukama, Bukoba-wadau


0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU