SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

23 February 2018

BALOZI DR KAMALA ATEMBELEA CHUO CHA UUGUZI MUGANA JANA FEBRUARY 22,2018

Siku ya jana Alhamisi Feb 22 alitembelea Chuo cha Uuguzi na Ukunga cha St. Magdalene Nursing school kilichopo Mugana Kata Bwanjai na kuzungumza na uongozi na wanafunzi wa chuo hicho.
Mara baada ya kupokea taarifa ya chuo kutoka kwa mkuu wa chuo hicho Sis.Lenatha Scarion, Balozi Dr.Kamala amewedhesha kwa kutoa kompyuta 5 na photocopy mashine 1 ya kisasa pamoja na kuzipokea changamoto nyingine pia ameahidi kutengeneza Uwanja wa Michezo na kutoa Vifaa vya michezo.
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na Viongozi wa Chuo hicho pamoja na Viongozi wa CCM Kata Bwanjai Wilaya Missenyi
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiagana na Kiongozi wa Chuo cha St. Magdalene Nursing school mara baada ya kuzungumza nao na kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha St. Magdalene Nursing school
 Mkuu wa Chuo cha St. Magdalene Nursing school Sis.Lenatha Scarion akisoma taarifa ya Chuo kwa Mgeni Rasmi Balozi Dr. Kamala
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Kamala akitoa neno
 Sehemu ya wanafunzi wa chuo cha Afya cha St. Magdalene Nursing school Mugana-Missenyi
Mbunge Balozi Kamala akiendelea kuzungumza na Uongozi na wanachuo wa Chuo cha Afya cha St. Magdalene Nursing school
Muonekana wa Jengo la Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Mugana Uuguzi na Ukunga cha St. Magdalene Nursing school kilichopo Mugana-Bwanjai Wilayani Missenyi.

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU