SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

17 February 2018

BALOZI DR KAMALA AWEZESHA UPATIKANI YA MASHINE YA KUKAMUA ALIZETI KIJIJINI MBALE

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala leo Februari 16,2018 ameendelea na ziara yake jimboni kwake pamoja na mambo mengine ameendeleza harakati za kuhamasisha kilimo cha alizeti kama zao la ziada la biashara amewezesha upatikanaji wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti pamoja na Mbegu za alizeti katika kijiji cha Mbale Kata Kitobo ikiwa ni jitihada za kuhamasisha maendeleo na kuunga mkono jitihada zinazoendelea za Serikali ya awamu ya tano za kujenga Tanzania ya Viwanda
Baadhi ya wananchi wakazi wa Kijiji cha Mbale Kata Kitobo wakimsiliza Mbunge wao.
 Mzee Joansen Kalokora Kato ambaye ni katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge akitoa utambulisho kwa wananchi msafara ulioambatana na mbunge
 Mtendaji wa Kata kitobo akikabidhi taarifa ya Kata kwa Mh. Mbunge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
 Diwani wa Kata Kitoba Mh.Willy Mtayoba akitoa hoja zake  na kubainisha kero zinazoikabili kata ya Kitobo,kikubwa alichokieleza ni hali ya kipato duni kwa mwananchi mmoja mmoja ndani ya kata yake
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ammeendelea na Ziara yake Jimboni kwa kutembelea Kijiji kimoja hadi kingine ikiwa ni uaratibu wake mara baada ya shughuli za Bunge na kabla ya kuelekea Bungeni
TAZAMA SEHEMU YA VIDEO HAPA CHINI

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU