SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

23 February 2018

LUGOYE SOCIAL CLUB WAKABIDHI MSAADA WA PHOTOCOPY MASHINE

 Mwakilishi wa Jumuiya ya Lugoye Social Club Mh. William Rutta Diwani wa Kata Ishozi kwa niaba ya wanalugoge wale wadau wakubwa wa maendeleo wanaozaliwa katika vijiji vya Ishozi ,Gera na Nshunju na makazi yao yakiwa Jijini Dar es Salaam wameendeleza upendo wao katika jamii kwa kutekeleza ahadi yao na kukabidhi msaada ya Photocopy mashine ya kisasa yenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu za Kitanzania (3,500,000/-) katika shule ya Sekondari Lugoye Wilayani Missenyi.
Ikumbukwe Decemba mwaka jana katika sherehe zao za kila mwaka tukio ambalo limekuwa likiambatana na na matendo ya huruma kwa kusaidia jamii inayo wazunguka hususani katika Vijiji Vyao.
Wanalugoye Wanaume walitoa ahadi ya msaada wa photocopy machine yenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu za Kitanzania (3,500,000/-) katika shule ya Sekondari ya Kata Ishozi ambayo sasa imetekelezwa na kukabidhiwa kwa Uongozi wa Shule hiyo kupitia kwa mwakilishi wao Diwani William Ruta.
Awali  Wanachama wa 'Lugoye Women Group' umoja wa Wanawake waliolewa na wana Lugoye katika sherehe za mwaka waliweza kukabidhi  msaada wa Computer na Printer katika shule ya Msingi Ishozi,msaada uliotokana na maombi ya kamati ya uongozi wa shule hiyo ili kuwezesha walimu kuchapisha ripoti za shule na kutunga mitihani ya wanafunzi wao.
Mh. William Ruta akikabidhiwa Cheti cha Shukrani
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ishozi wakifurahia Camera ya Bukobawadau,awali shule hiyo ilikabidhiwa msaada ya Printer na Kompyuta kutoka kwa wanachama wa 'Lugoye Women'
Taswira mazingira ya shule ya Msingi Ishozi
Mwanahabari Lilian akiongea na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lugoye
Barua ya Shukrani

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU