SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

16 February 2018

UZINDUZI WA KITUO CHA #CSIBUKOBA

 Uzinduzi wa taasisi ya #CSIBukoba yenye lengo la kusaidia makundi mbalimbali wakiwemo mayatima ,wajane na watu wasiojiweza pamoja na masikiti umefanyika Jana Feb15,2018 katika kituo cha Nusra yatima kilichopo Kata ya Kashai Manispaa Bukoba Uzinduzi huo umeambatana na ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho
 Baadhi ya Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madaftari, vitabu ,Kandambili,sare za shule nk
Mjumbe wa Taasisi ya #CSIBukoba Mwalimu Hamidu Kumungoma pichani kulia  akitolea jambo ufafanuzi
Mwenyekiti wa Kituo cha Nusra Yatima Bwana Bashir Kabyemela pichani kushoto alitoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa kusaidia watu wasiojiweza ili kupunguza makali ya maisha kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Haji Abuba Sued akitoa neno katika uzinduzi wa kituo hicho
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha #CSIBukoba wakipata huduma ya chai
 Sheikh Idrisa akitoa Dua mara baada ya kukamilika kwa usinduzi wa shughuli ya taasisi ya #CSIBukoba
Muendelezo wa matukio ya picha
 Mjumbe akitoa mchango wake wa mawazo katika kuendeleza harakati ya kusaidia jamii ya wasiojiweza
Katika picha ya pamoja na Mama Nurumlezi wa kituo cha Nusura yatima kilichopo Kashai NANISPAA Bukoba.

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU