SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

16 February 2018

WAZIRI NDALICHAKO AKIWA MKOANI KAGERA AAGIZA MAAFISA ELIMU NCHINI KUDAHILI WANAFUNZI KULINGANA NA UWEZO WA MIUNDOMBINU YA SHULE

 Waziara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kuanzia Februari 13 hadi 14, 2018 alitembelea, kukagua na kupokea miradi mbalimbali ya Elimu ikiwa ni pamoja na kutembelea baadhi ya shule za Sekondari na kuonge na wanafunzi wa shule hizo.
 Wilayani Muleba Katika siku yake ya kwanza Mkoani Kagera Prof. Ndalichako alitembelea na kukagua miundombinu ya Chuo cha Ualimu Katoke Wilayani Muleba ambapo katika chuo hicho ambacho miundombinu yake imechoka na alihaidi kuwa kitatengewa bajeti ya ukarabati kuanzia bajeti ya mwaka 2018/2019 ili kikarabatiwe.
Shule ya Sekondari Profesa Joyce Ndalichako, Prof. Ndalichako pia alifika katika shule hiyo iliyopewa jina lake ili kujionea ujenzi wa shule ambayo fedha zake zilitolewa na Serikali, Katika Shule hiyo Prof. Ndalichako aliridhika na viwango vya ujenzi wa shule hiyo na kuwapongeza wananchi kushirikiana na Serikali katika kujenga Shule hiyo.
 Prof. Ndalichako aliwahasa wanafunzi kujitahidi katika masomo yao ili wasimwangushe kwani shule hiyo inaitwa jina lake. Pia alihaidi kutoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya kujenga Maabara na shilingi milioni 3 kwajili ya kununulia vitabu ili wanafunzi wa shule hiyo waweze kupata elimu stahiki.
Shule ya Sekondari Prof. Anna Tibaijuka Muleba mjini, katika ziara yake pia Prof. Ndalichako pia lipata wasaa wa kuitembelea Shule hiyo ambayo bado ina changamoto ya miundombinu kama madarasa pamoja samani za viti na meza kwa ajili ya wanafunzi .
 Agizo; Baada ya kuona msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo Prof. Ndalichako alitoa Agizo kwa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya Nchini kuacha tabia ya kudahili wanafaunzi juu ya uwezo wa miundombinu katika shule husika. Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya popote nitakapokuta wamedahili watoto kuzidi uwezo wa miundombinu iliyopo watawajibika wao wenyewe, Alisistiza Prof. Ndalichako.
Prof. Ndalichako alisema kuwa ni ajabu kuona shule haina madarasa ya kutosha alafu Maafisa Elimu wanawapeleka wanafunzi wengi katika shule hiyo ambayo haiwezi kuwamudu wanafunzi hao kwa wakati mmoja. Katika hatua nyingine Prof. Ndalichako alihaidi kutoa mabati 100 ili kumalizia chumba cha darasa ambalo ujenzi wake unaendelea.
 Wilayani Missenyi Siku hiyo hiyo akiwa Wilayani Missenyi Prof. Ndalichako alitembelea Chuo cha Maendelea ya Wananchi Gera na kujionea ukarabati wa Chuo hicho ambapo Serikali ilitoa Shilingi Milioni 75 ili kukarabati baadhi ya majengo. Prof. Ndalichako hakuridhishwa na kiwango cha ukarabati uliofanywa na VETA Kagera katika chuo hicho kwani haundani na thamani ya fedha iliyotolewa.
Waziri Ndalichako aliwakemea VETA nchini kuwa wamekuwa wakifanya kazi zao chini ya kiwango na alisema kuwa atatuma ukaguzi maalum katika Chuo hicho ili kukagua kazi iliyofanyika na kama ikigundulika kuwa kuna uchakachuzi VETA Kagera watalazimika kukiarabati chuo hicho kwa gharama zao wenyewe, pia ukaguzi huo maalum utapitia na shughuli zao za kawaida kwani ilionekana kuwa wamekuwa wakifanya madudu.
Na: Sylveste Raphael

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU