SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

28 February 2018

ZIARA YA MBUNGE BALOZI KAMALA KATA GERA

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza na wananchi wa Gera katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini Hapo,Balozi Kamala amechangia miradi ya maendeleo na Vikundi vya Ujasiriamali vya ufukaji wa Samaki na kilimo cha mboga mboga.
Mratibu Elimu kata akisoma taarifa ya Kata ya Gera.
 Mbunge Balozi Dr. Kamala akipokea taarifa ya kata
 Pichani kushoto ni Mwalimu Bitegeko Diwani kata Gera akipokea waraka wa Elimu bure kuhusu elimu msingi bila malipo, Swala la Elimu bure limeendelea kuzua tafsiri potofu na kuuchukua sura mpya juu ya mustakabali wa elimu hususani katika Jimbo la Nkenge ,Balozi Dr Kamala anajikita zaidi kuwaeleza wananchi Katika kila mkutano wake umuhimu wa Wazazi kuchangia kwa hiari wasishindwe kuchangia ata Uji mashuleni kwani katika waraka huo michango haijakatazwa kabisa,Kauli hiyo imejikita kwenye Waraka namba 3 wa mwaka 2016 ambao umeainisha majukumu ya wadau mbalimbali wakiwemo wazazi ambao wana wajibu wa kuchangia sehemu ndogo ya michango kwenye shule za msingi.
Wadau katika hali ya usikivu
 Baadhi ya wamanchi wakimsikiliza mbunge wao Balozi Dr. Kamala
Pichani ni sehemu ya kikundi cha kinamama wakiwa tayari kubabidhi zawadi kwa mbunge wao Balozi Dr. Kamala
Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala Mbunge Jimbo la Nkenge akipokea zawadi kutoka kwa Vikundi vya akinamama Kata Gera Wilayani Missenyi mara baada yamkutano wake wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Kila kijiji,kila kata na baadhi ya Vitongoji jimboni,Jimbo la Nkenge lina jumla ya kata 20.
 Balozi akishukru kwa zawadi alizopokeaWananchi wakimsikiliza Mbunge Balozi Dr. Kamala Balozi Kamala akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kilimo cha Alizeti kama zao la ziada la biashara.

 Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala Mbunge Jimbo la Nkenge akikagua zahanati ya Kata Gera
 Mradi wa Jengo la Ofisi ya Kata Gera

 Ukaguzi wa hatua zilizofikiwa Ujenzi wa Ofisi ya Kata, Balozi Kamala ameweza kuchangia Kiasi cha sh. Milioni moja

Mbunge akibadilishana mawazo na wadau kuhusu suala la mgogoro wa ardhi lililopo kata eneo hilo

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU