SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

02 March 2018

JENEZA LENYE MWILI WA BI MASTIDIA K.BARUTI LIKIWASILI UWANJA WA NDEGE MJINI BUKOBA

Simanzi kbwa kwa Wanafamilia na ndugu wa karibu wakitokwa na machozi baada ya kuona Jeneza lililobeba mwili wa mpendwa wao Bi Mastidia Baruti likiwasili Uwanja wa ndege mjini Bukoba asubuhi ya leo Alhamisi March 1,2018
Pata matukio ya picha wakati Waombolezaji wakisubiri mwili kuwasili kutoka Jijini Dar es Salaam,Shughuli ya mazishi inatalajiwa kufanyika siku ya Jumamosi March 3,2018 mchana Nyumbani kwao Mugeza-Burugo.
Tunamuombea apumzike kwa Amani .Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe amen!
 Ndugu wa familia wakitokwa na machozi mara baada ya kuwasili kwa Mwili wa mpendwa wao Bi Mastidia K. Baruti
Mpendwa Bi Mastidia Baruti  pichani enzi za uhai wake
 Waombolezaji wakimfariji Ndugu Ruga Baruti kwa msiba huu wa mama yake mpendwa.Bi Bi Mastidia Baruti.
 Mzee Baruti (Nkango) na mtoto wake Ruga Baruti wakitokwa machozi mara baada ya kukutana Uwanjani hapo
 Umati wa waombolezaji waliofika kupokea mwili wa Bi Bi Mastidia Baruti  aliyefariki juzi Feb 27,2018 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu
 Sheikh Haruna Kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera akiwa ameongozana na waombolezaji katika shughuli ya kuupokea mwili wa Mke wa rafiki yake Mzee Baruti,Bi Bi Mastidia Baruti wakati ukiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa Bukoba
 Mama Muhazi akimfariji mfiwa kwa msiba huu mkubwa wa kuondokewa na mama yake mzazi
 Mzee Enesmo Niyegila na Mama Muhazi pichani
Muendelezo wa matukio ya picha
 Jeneza limewasili na Ndege aina Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania 
 Taswira mbalimbali nje ya Uwanja ya Ndege Mjini Bukoba.
 Uncle Majid Kichwabuta na Mr Rahym Kabyemela wakiwa wameungana na waombolezaji wengine.
 Waombolezaji wakielekea msibani
 Msafara ukielekea nyumbani kwa familia Maeneo ya Mugeza
 Nyumbani Kijijini Burugo-Mugeza nje kidogo ya mji wa Bukoba.
 Vilio na machozi vikitawala kwa wanafamilia
Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu Bi Mastidia Baruti
 Masikani kwa Ruga Baruti Kijijini Burugo-Mugeza
Kijana Rama Issa akiwasili msibani hapo.
BUKOBAWDAU TUNATOA POLE KWA WANAFAMILIA KWA KUONDOKEWA NA MPENDWA WAO BI MASTIDIA BARUTI BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA.....JINA LAKE LIHIMIDIWE!!

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU