SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

04 April 2018

BALOZI KAGASHEKI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA JUMUIA YA WAZAZI CCM WILAYA BUKOBA

Umati wa wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi CCM Wilaya Bukoba wakimlaki Mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki aliyeshiriki maadhimisho ya wiki hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za Kijamii ikiwemo kupanda Miti katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Hamugembe na kuzinda vikundi mbalimbali vya akina mama wajasiriamali wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya Mkoa Kagera  Haji Abbubakar Sued akiongozani na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Rahel Ndegereka kumkaribisha Mgeni Rasmi wa Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi Wilaya Bukoba Balozi Khamis Sued Kagasheki wakati akiwasili katika Ukumbi wa Linas Club Kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Jumuia hiyo uliofanyika leo Jumanne April 3,2018.

 Mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi Wilaya Bukoba aliyekwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki akiongozana  na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba Mganyizi Zachwa Muendelezo wa matukio ya picha kutoka ndani ya Ukumbi wa Linas Club


Wiki ya Jumuia ya wazazi wilaya BukobaEndelea kuwa nasi mpaka mwisho kupata yaliyojiri katika hafla hiyo pia matukio mengine zaidi unaweza kujiunga katika kurasa zetu za facebook na Instagram @bukobawadau. 
Baadhi wa wananchi wakifatilia kinachojiri katika hafla ya maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi Wilaya Bukoba

Shairi kwa Mgeni Rasmi
 Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Kagera Amimu Omary akiongea na umati uliohudhuria maadhimisho ya wiki ya Jumuia ya wazazi Wilaya Bukoba leo April 3,2018

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Kagera Amimu Omary akimpokea Mwanachama mpya aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa Ijuganyundo A kupitia chama cha wananchi  (CUF) Justuce Abdallah aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. 


Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba Mganyizi Zachwa akitumia vyema fursa aliyopewa na kuongea na halaiki iliyohudhuria hafla ya maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi Wilaya Bukoba

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba Mganyizi Zachwa akiongea na umati uliohudhuria siku ya maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi Wilaya Bukoba , pamoja na mambo mengine Mh Mganyizi awahasa wanaccm  Bukoba kudumisha mshikamano.


Hakika watu ni wengi kweli kweli

Bwana Yazid mwenezi wa CCM Wilaya Bukoba wakati akitoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali wa Chama Wilaya ya Bukoba

Hamsha hamsha kutoka kwa mwenyekiti ya UVCCM Wilaya Bukoba

 Haji Abbakar Sued Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Mkoa Kagera akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa Kagera.


Haji Abubakar Sued akiongea katika hafla hiyo.

Muendelezo wa matukio ya picha


Nyomi ya watu ukumbini si kawaida.

Taswira mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Linas
Taswira ndani ya Ukumbi wa Linas maadhimisho ya Wiki ya Wazazi wilaya Bukoba.

 Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Rahel Ndegereka akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti waCcm Mkoa Kagera katika sherehe za maadhimisho ya wiki ya Jumuia ya wazazi Wilaya Bukoba Mama Ruby mjumbe wa wa Balaza kuu la Jumuia ya Wazazi akifatilia kinachojiri ukumbini hapoAkiongea na wananchi Balozi Kagasheki ametumia fulsa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kusimamia na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuimarisha Usafiri wa anga ,Balozi amepongeza kuwasili kwa ndege nyingine ya 3 aina ya Bombardier Q 400 mpya kabisa na ya kisasa.

Mzee Zachwa Mganyizi akiteta jambo na Bi Rahel Ndegereka Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba 

Mh. Balozi Hamis Kagasheki akiendelea kuzungumza na halaiki iliyojitokeza katika maadhimisho hayo.Mdau akichangia vikundi vya wanawake wajasiriamali shughuli iliyokuwa ikiongozwa na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Rahel Ndegereka


Bwana Mkhusin Kichwabuta na mtaalam Al Amin Abdul wakiwa na mshangao kufatia watu wanavyo sukumana kwa ajili ya kumsalimia Balozi Khamis Kagasheki

Ni Swahiba Balozi Khamis Kagasheki aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba akiendelea kusalimia na wananchi waliofika kwa wingi katika shughuli ya maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Wilaya Bukoba

Salaam za hapa na mara mara baada ya kuongea na wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Ukumbi wa Linas Club #maadhimishoyaWikiyaWazaziWilayabukoba.

Watu wakionyesha mahaba kwa mgeni Rasmi Balozi Khamis Kagasheki


Burudani kutoka kwa msanii Kamdingi.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nshomile akifanya yake katika maadhimisho hayo ndani ya ukumbi wa Linas Club

 Balozi Kagasheki akipanda mti katika mazingira ya Shule ya Msingi Kashabo iliyopo katika kata ya Hamugembe Manispaa ya Bukoba katika maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Wilaya Bukoba yaliyofanyika leo April 3,2018

Mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi Wilaya Bukoba Balozi Khamis Kagasheki akiwa katika picha ya pamoja na Bi Leonida Muhazi kata wa Chama cha mapinduzi CCM

 Picha inaongea watu wakionyesha furaha kukutana na Balozi Kagasheki tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015 na leo amefika kwa ajili ya shughuli maalum ya kushiriki kama mgeni Rasmi wa maadhimisho ya wiki ya Jumuia ya Wazazi Wilaya Bukoba yaliyoandaliwa na Kata ya Hamugembe ki wilayala ambapo siku ya Kesho yatafanyika kimkoa huko Wilayani Missenyi

 Picha unaongea ...


 Ni mwendo wa Selfie kila mtu akihitaji picha na Balozi Kagasheki

Umati huu ukimsindikiza Balozi Kagasheki mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hafla ya maadhimisho ya wiki ya Jumuia ya wazazi Wilaya Bukoba


 Kivutio kikubwa katika maadhimisho hayo ni Uwepo wa Balozi Kagasheki kama unavyoweza kujionea umati wa watu ukiwa umezunguka gari lake wakati anaondoka ukumbini hapo


 Umati ukiwa umezunguka gari la Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Jumuia ya Wazazi aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki

 Wananchi wakiagana na Balozi Kagasheki nje ya ukumbi wa Linas Club Muendelezo wa matukio ya picha #maadhimishoyaWikiyaWazaziWilayabukoba

Mwisho wa matukio yaliyojiri siku ya  #maadhimishoyaWikiyaWazaziWilayabukoba kutoka ukumbi wa Linas Club April 3,2017.


0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU