SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

25 April 2018

BUKOBA:JESHI LA POLISI LATOA ONYO KWA WATAKAOANDAMANA

 BUKOBA: Vikosi vya ulinzi na usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya utayari ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mazoezi yao ya kila siku huku wananchi wakiaswa kufata sheria na kanuni za nchi ili kuhakikisha amani na usalama vinakuwepo katika maeneo yao.
Mazoezi hayo yameanzia katika ofisi za mkuu wa mkoa kagera na kuzunguka mitaa mbalimbali ya manispaa ya bukoba na kuhitimishwa katika viwanja vya wazi vya gymkhana vilivyopo katika fukwe ya ziwa Victoria.
Akiongea mala baada ya Mazoezi hayo kamanda wa polisi mkoani Kagera RPC Agustine Ollomi amesema kuwa mazoezi hayo ni ya kawaida kwa vikosi vyote vya ulinzi na usalama katika mkoa huu ambayo wamekuwa wakiyafanya kila siku za juma Mosi ambayo huwajumuisha wananchi wa kawaida pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama.
 Kuhusiana na suala la vuguvugu la maandamano yanayopangwa kufanyika April 26 mwaka huu linalozagaa mitandaoni kamanda Ollomi amesema kuwa Jeshi la polisi mkoani Kagera lipo timamu na kamilifu pamoja na vikosi vingine vya ulinzi na usalama katika kumkabiri yeyote atakayejitokeza kufanya maandamano haramu ambapo amesisitiza kuwa hakutokuwa na mzaha katika kuwashughurikia wale wote watakao kaidi amri halali ya polisi.
 Hata hivyo kamanda Ollomi amevithibitishia vyombo vya habari kuwa hajapata taarifa wala barua ya kumuomba kibari cha maandamano yoyote katika mkoa wake wa kagera na kuongeza kuwa hata kama wangelipata barua ya kuomba kibali kuhusiana na maandamano hayo wangeangalia hali ya usalama na madhumini ya maandamano hayo, huku akiwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku na kusisitiza kuwa hali ya usalama katika mkoa wa Kagera ni shwari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera AGUSTINE OLLOMI akiongea na vyombo vya Habari mala baada ya kumaliza kufanya mazoezi.
Kwa matukio na habari za Papo hapo follow @bukobawadau
Photo credit @allawi.

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU