SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

17 April 2018

MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA MARUKU,KAGERA

 Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Respicius DIOCLESS mkazi wa kijiji Bulambizi Kata KANYANGEREKO, Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera, Amewaua watoto wake wawili mapacha Deonidas Respicius na Diocress Respicius (miaka mine) kwa kuwachinja na kuwatenganisha vichwa na viwiliwili, tukio lililotokea usiku wa kuamkia jumapili ya 15 April 2018.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambae pia ni mtoto mdogo wa kumzaa, KELVIN RESPICUS (miaka minne, na mtoto wa mwanamke mwingine) amesema usiku wa tukio baba yake mzazi aliwachukua marehemu hao kwa zamu na kIsha kutelekeza mauaji hayo, na alipojaribu kuhoji walipo ndugu zake alijibiwa kuwa wapo mbinguni.
 Muonekano wa makaburi  ya walipozikwa mapacha hao waliochinjwa na Baba yao mzazi
 Taarifa zinaeleza kuwa kabla ya tukio, mtuhumiwa allikuwa akiishi na watoto wake watatu ambao mapacha Hao aliwazaa na mama anaejulikana kwa jina la Deovitha David mkazi wa ambae kwa sasa wamekwisha tengana na kubaki kama mzazi mwenzake.
Duru zinazidi kueleza kuwa marehemu hao mapacha kabla ya mauti kuwafika, mama yao alimuomba mzazi mwenzake kuja kuwachukua wanae wakamtembelee na kIsha atawarejesha, mtuhumiwa alimkubalia mzazi mwenzake na kumtaka awarejeshe watoto hao Jumamosi ya tarehe 15 April, na baada ya mapacha hao kuwa wamerejeshwa, mama huyo aliondoka zake ambapo Tukio la la mauaji hayo lilifanyika usiku huo wakati mama huyo akiwa tayari amekwisha rejea katika mji wake.
Kisa kamili cha mauaji hayo mpaka sasa hakijajulikana japo inahusishwa na mgogoro wa kimapenzi uliokuwa ukiendelea kati ya wanandoa haona wengine wakihusisha na kile walichokiita wivu wa mapenzi. Juhudi za kutaka kuhahamu ukweli kutoka mama wa marehemu zimeshindikana mpaka sasa kutokana na majonzi na huzuni mkubwa uliopelekea mama huyo kushindwa kabisa kuongea na vyombo vya habari.
HOFU YA WANAKIJIJI. Toka usiku wa tukio, kulipopambazuka mtoto ndiye alikuwa wa kwanza kutoa taarifa kwa ndugu jamaa na majirani ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa kijiji Bulambuzi ndugu , baada ya taarifa kusambaa kuhusu mauaji hayo mtuhumiwa alifanikiwa kukimbia kusikojulikana lakini ikisemekana kuwa alikuwa bado yumo ndani ya kijiji hicho, wanakijiji baada ya tukio hilo, wamechukua hatua ya kuchoma moto nyumba ya marehemu na kukata mazao ikiwemo migomba na kisha kuanza msako mkali wa kumsaka muuaji huy. Huku hayo yakiendelea jambo la kushangaza ni kuwa, Muuaji huyo kwa ujasiri mkubwa amekuwa akituma ujumbe mfupi na hata kupiga simu kabisa kwa baadhi ya watu akitoa maelekezo kuwa wasihangaike kumtafuta kwani tukio hilo kalifanya akiwa na akili timamu, na akikamilisha azma yake atajisalaimisha, kitu amabacho kimezua hofu kubwa kwa wanakijiji wakihofia kuwa, huenda muuaji atarudi kufanya Tukio jingine zaidi hasa kwa wale wanaojaribu kumfatilia.
Mpaka tunaondoka eneo la tukio tayari muuaji huyo amekwisha kamatwa Jijini Mwanza na taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanyika, huku miili ya marehemu hao tayari imeruhusiwa kuzikwa.
Baadhi yawaombolezaji wakifa msibani hapo
Matukio ya video yanapatikana kupia akaunti yetu ya Instagram @bukobawadau
Credit:ABDULLATIF YUNUS

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU