SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

09 June 2018

PASIPOTI ZA KIELEKITRONIKI ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KAGERA NA KUTOLEWA KWA MARA YA KWANZA KWA WANANCHI WA KAGERA

Mkoa wa Kagera wazindua Rasmi Pasipoti za Kielekitroniki leo Juni 8, 2018 katika viwanja vya Uhuru Manispaa ya Bukoba ambapo Pasipoti hizo zimezinduliwa na kutolewa kwa mara ya kwanza  Mkoani Kagera kwa Viongozi na Wananchi wa kawaida na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mkuu wa wa Wilaya ya Bukoba  Mhe. Deodatus Kinawilo.
Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu  Mhe Deodatus Kinawilo akizindua Pasipoti za Kielekitroniki katika viwanja vya Uhuru alisema kuwa Mkoa wa Kagera unajivunia kuzindua wa  Pasipoti za Kielekitroniki  kwani sasa wananchi wake watapata Pasipoti zinazotambulika Kimataifa na zenye uhakikaka zaidi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa Mhe Kinawli Akimkabidhi Pasipoti ya Kielekitroniki Baba Askofu Lwoma wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Bukoba
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Kinawilo Akimkabidhi Pasipoti ya Kielekitroniki Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Luyango
Kamishna wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga (Kushoto) Akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kinawilo  Pasipoti ya Kielekitroniki Baada ya Uzinduzi
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo Akisoma Hotuba ya Uzinduzi wa Pasipoti ya Kielekitriniki Mkoani Kagera Kwaniba ya Mkuu wa Mkoa
Sheikh Haruna Kichwabuta Sheikh Mkuu wa Mkoa Kagera akisoma Dua ya uzinduzi wa Pasopoti za Kielekitroniki
Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Wakisikiliza Kwa Umakini Hotuba ya Uzinduzi wa Pasipoti za Kielekitroniki Mkoani Kagera
Katibu Tawala Mkoa Kagera CP Diwani Athuman Akisubiri Kuchukuliwa Alama za Vidole Kukamilisha Hatua za Pasipoti ya Kielekitroniki
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Kijuu na Katibu Tawala Mkoa CP Diwani Athuman Wakishiriki Hatua za Kupata Pasipoti ya Kielekitroniki
Kamishna wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga Katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Dini walioweza kujipatia mapema Pasipoti za Kielekitroniki
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoriki la Bukoba Desiderius Lwoma na Askofu Msaidizi Kilaini Wakifurahia Pasipoti zao za Kielekitriniki Baada ya Kuzinduliwa Rasmi na Kukabidhiwa
Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoriki la Bukoba Akitoa Neno la Shukrani Baada ya Uzinduzi na Kukabidhiwa Rasmi Pasipoti za Kielekitroniki Mkoani Kagera
 PASIPOTI ZA KIELEKITRONIKI ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KAGERA NA KUTOLEWA KWA MARA YA KWANZA KWA WANANCHI WA KAGERA
Mkoa wa Kagera wazindua Rasmi Pasipoti za Kielekitroniki leo Juni 8, 2018 katika viwanja vya Uhuru Manispaa ya Bukoba ambapo Pasipoti hizo zimezinduliwa na kutolewa kwa mara ya kwanza  Mkoani Kagera kwa Viongozi na Wananchi wa kawaida na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mkuu wa wa Wilaya ya Bukoba  Mhe. Deodatus Kinawilo.
Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu  Mhe Deodatus Kinawilo akizindua Pasipoti za Kielekitroniki katika viwanja vya Uhuru alisema kuwa Mkoa wa Kagera unajivunia kuzindua wa  Pasipoti za Kielekitroniki  kwani sasa wananchi wake watapata Pasipoti zinazotambulika Kimataifa na zenye uhakikaka zaidi.
Mhe. Kinawilo alisema kuwa Pasipoti ya Kielekitroniki inayo mambo muhimu makuu manne tofauti na Pasipoti  ya zamani kama ifuatavyo; Kwanza, Ni pasipoti inyomtambulisha Mtanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kimataifa,  kwahiyo Pasipoti ya Afrika Mashariki haitatolewa tena bali itatumika Pasipoti  moja ya Kielekitroniki tu.
Pili, Pasipoti ya Kielekitroniki inazo alama za kiusalama ambazo si rahisi kuzigushi. Tatu, Pasipoti ya Kielekitroniki ni ya Kimataifa ambayo hahitaji ulazima wa ukaguzi bali mtu mwenye nayo anaweza kupita kwenye mitambo maalum na kujulikana kuwa ni Mtanzania. Nne, Pasipoti ya Kielekitroniki inayo program maalum ambayo mwananchi anaweza kuitunza kwenye simu yake na kama Pasipoti yake ikipotea ghafla anaweza kuitumia aliyoitunza kwenye simu yake.
Mwisho Kaimu Mkuu wa Mkoa Mhe. Kinawilo alitoa tahadhari kwa Watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa makini wakati wa kutoa Pasipoti za Kielekitroniki kwa wananchi ambao ni Watanzania tu na siyo kuzitoa kwa wasio raia wa Tanzania. Pia alitoa wito kwa Maafisa wa Idara ya Uhamiaji kuwasaidia wananchi watakaohitaji Pasipoti hizo na hawana uelewa wa kutumia kompyuta ili wasaidiwe kujaza fomu zao.
Katika upande mwingine Kamishina wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga alisema kuwa mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuzindua Pasipoti za Kielekitroniki Januari 31, 2018 Pasipoti hizo zilikuwa zinatolewa Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam na Zanzibar tu lakini sasa mikoa imeanzi kuzindua na kutoa Pasipoti za Kielekitroniki.
Kamishna Kihinga alisema kuwa tayari Pasipoti za Kielekitroniki zimeanza kutolewa katika mikoa ya Dadoma, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na sasa Mkoa wa Kagera ambao uzinduzi umefanyika leo Juni 8, 2018. Jumla ya Pasipoti za Kielekitroniki 17,595; zimetolewa  Pasipoti za Kielekitroniki za kawaida zikiwa 17,289 za Utumishi 56, za Kidiplomasia 248, na Diplomasia Maalum mbili tu.
Naye Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Kagera Abdalah Towo akiongea na mhadhara wa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Pasipoti za Kielekitroniki aliwakumbusha Maafisa wenzake katika Wilaya kuwa Elimu imetolewa ya kutosha kwao na ni lazima kuwaelimisha wananchi na kuwaongoza katika kupata Pasipoti za Kielekitroniki katika Wilaya zao.
 Pia Bw. Towo alitoa rai kwa wananchi waliopatiwa Pasipoti za Kielekitroniki katika uzinduzi huo kuwa mabalozi wazuri wa kuwaelimisha wenzao na kuhakikisha wanapitia michakato yote wao waliyoipitia na kama kutatokea mwananchi anasema yeye hajapitia mchakato huo na amepata Pasipoti ya kielekitroniki aripotiwe mara moja katika Ofisi za Uhamiaji ili hatua zichuliwe mara moja.
Aidha, Bw. Towo alisema katika uzinduzi huo zilitolewa Pasipoti za Kielekitroniki 101 kwa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini, Wazee, Watumishi na Wananchi. Rai kwa wananchi kwa kuwa Mkoa wa Kagera umepakana na nchi tatu ni lazima wananchi kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa ili Pasipoti za Kielekitroniki zisitolewe kwa wasiokuwa raia wa Tanzania.
Kwaniaba ya Viongozi na wote waliopatiwa Pasipoti za Kielekitroniki katika uzinduzi Mkoani Kagera Baba Askofu Methodius Kilaini  Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoriki la Bukoba aliishukuru Serikali na Idara ya Uhamiaji kwa kutoa Pasipoti za Kielekitroniki kwa wananchi na alisema kuwa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera imejipanga vizuri hasa katika mapokezi ya wananchi na huduma.
“Tunashukuru sana na nimeikagua Pasipoti yangu ya Kielekitroniki na kugundua kuwa ni pasipoti nzuri sana tena  sana, sasa itatusaidia sisi kama Viongozi wa dini na wananchi katika kusafiri, naiona Tanzania ikiendana na mataifa mengine katika masuala ya mitandao.” Alisistiza Baba Askofu Kilaini
Unahitaji nini ili Upate Pasipoti ya Kielekitroniki?
Gharama ya Pasipoti ya Kielekitroniki ni Shilingi 150,000/=, Utajaza fomu hata ukiwa nyumbani ambayo inapatikana katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.Immigratino.go.tz . Viamabatanisho ni pamoja na Kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa cha kwako na cha mzazi wako mmoja, Barua ya utambulisho kutoka kazini kwako/Mtendaji wa kata, Kitambulisho cha Kazi/mpiga kura, na picha tatu pasipoti size.

MWISHO

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU