SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

29 July 2018

KILIMO CHA ALIZETI KYAKA - MISSENYI

 Alizeti  hulimwa kwa wingi karibu maeneo yote nchini Tanzania ,Pia mkoani Kagera Wilayani Missenyi zao hili linakubali sawa na maeneo mengine ya nyanda za kaskazini, kati na mashariki na hii inatokana na uwezo wa alizeti kustawi vizuri katika mazingira mengi tofauti bila ya kuwa na utofauti mkubwa katika uzalishaji wake.
Zao la Alizeti hulimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ambapo baadhi yake ni kama vile kutengeneza mafuta, kulishia mifugo na matumizi ya viwandani pichani Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mh.Balozi Dr. Kamala akiwa shambani kwa Bwana Ismail Ramadhani kwa ajili ya kujionea mavuno ya shamba la mkulima hilo
Balozi Dr Kamala pichani akitazama Kichwa cha alizeti yenye ubora baada ya kukomaa na kuvunwa , pichani kushoto ni Bibi Kilimo wa Kata ya Kyaka na kulia kwake ni Afisa kilimo wa Wilaya ya Missenyi
Bi Khadja pichani katikati ambaye ni Mkulima wa Shamba hilo lililopo maeneo ya Kyaka Wilayani Missenyi akimuelezo Mbunge wake Balozi Dr.Kamala baadhi ya Changamoto wanazokumbano nazo katika kilimo cha Alizeti
 Alizeti pia huweza kulimwa katika mfumo wa kilimo mseto ambapo zao la mahindi ndilo linalopendekezwa hasa kulimwa mseto na alizeti kwa sababu mazao haya mawili yana mfanano mkubwa katika matunzo na muda wa ukuaji hadi kukomaa. Katika kilimo mseto cha alizeti na mahindi panda mbegu za mahindi na alizeti katika mistari iliyo katika mpangilio wa mistari miwili miwili au mmoja mmoja ya alizeti na mahindi katika nafasi ya sm 75 kwa sm 30 katika shamba moja.
Kutengeneza Mafuta
Mbegu za Alizeti zinapokamuliwa hutoa mafuta yanayoweza kutumika kwa matumizi mbalimbali hasa kupikia. Wataalamu wengi wa afya wanapendekeza matumizi ya mafuta ya alizeti katika mapishi kwa sababu hayana lehemu (cholesterol) na hivyo ni salama kiafya hasa yanapotumika vizuri. Kwa sababu hiyo mafuta yanayotokana na alizeti yamekuwa na soko zuri na hivyo biashara yake ni njia nzuri ya kumwongezea mkulima na mfanyabiashara kipato.
Kulishia Mifugo
Mashudu yanayotokana na alizeti baada ya kukamua mafuta ni chakula kizuri kwa kulishia mifugo kama vile ng’ombe wa maziwa, mbuzi, nguruwe, kuku au sungura kwa sababu yana kiasi kikubwa cha protini na mafuta na kiasi cha nyuzi nyuzi muhimu kwa mmeng’enyo wa chakula kwa wanyama.
Matumizi ya Viwandani
Mafuta yanayotokana na alizeti pia yanaweza kutumika katika utengenezaji wa sabuni, rangi na vipodozi mbalimbali. Vile-vile viwanda vya kutengeneza karatasi hutumia baadhi ya sehemu za mmea wa alizeti kama malighafi katika utengenezaji wa karatasi.

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU