SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

24 August 2018

BALOZI DR KAMALA KAMPENI UCHAGUZI MDOGO UDIWANI KATA MINZIRO WILAYANI MISSENYI

 Balozi Kamala aongoza Kampeni za Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Minziro na kumnadi mgombea udiwani wa Kata hiyo kwa tiketi ya (CCM) Frances Henery Mutaasa.
Katika kampeni hizo zilizofanyika jana jioni kwenye eneo la Kijiji cha Rugazi,Balozi Kamala aliwaomba wakazi wa eneo hilo kumchagua Mutasaa ili kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi zake za kufanikisha maendeleo ya wananchi, hasa miradi mikubwa anayoianzisha nchini. “Maendeleo yote yanayofanyika nchini ni utekelezaji wa ilani ya CCM, hivyo msipotoshwe wanaojinadi kuwa watatekeleza mambo ya maendeleo, hiii miradi ya Umeme na Maji tuliyoipata Missenyi ni kazi ya Rais Magufuli,” alisema.
TAZAMA SEHEMU YA VIDEO HAPA CHINI
 Kwa sasa tumepata mradi mkubwa wa maji ya bomba kutoka ziwa Victoria katika vijiji vya Bukwali, Bushago, Kashenye, Kigarama Bweyunge, Bugombe,na Kikukwe pia kuna mradi wa pili wa bomba la maji katika vijiji vya Ishunju, Kyelima, Katolelwa na Luhano alisema" Balozi Dr Kamala katika mkutano huo uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa Kagera na viongozi wa Chama Wilaya Missenyi.

Mwisho

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU