SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

01 August 2018

BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTOMbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dr.Deodorus Kamala ametoa kiasi cha shilingi (milioni tano na laki sita ) 5,600,000/-kwa ajili ununuzi wa masanduku ya kubebea vifaa vya huduma ya kwanza (First Aid Kit) kwenye zahanati 10 za Halmashauri ya Missenyi,Masanduku hayo yakiwa na vitu muhimu vinavyohitajika kwa dharula mbalimbali.
Dr.Diodorus Buberwa Kamala amesema hayo alipofanya ziara katika Vituo vya Afya na zahanati kujionea changamoto na hali ya uwepo wa dawa na kuweka mikakati ya ufumbuzi katika huduma za Mama na Mtoto,Katika ziara hiyo ameongozana na Meneja wa MSD kanda ya Kagera na Geita Bwana Egidius Rwezaula .

Amezitaja Zahanati zilizopewa (First Aid Kit) ni Kashanga, Buyango, Bugandika,Kitobo, Kanyigo,Minziro ,Kyaka,Kilimilile,Bugorora pamoja na Kakindo .
Balozi Kamala amepongeza hali ya utoaji na ubora wa huduma za afya Wilayani Missenyi na kuwapongeza MSD kwa kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa huduma za Afya kupatikana .

Kwa upande wake Meneja wa Msd kanda ya Kagera na Geita Egidius Rwezaula amesema kuwa kazi ya kuyafikisha masanduku hayo kwenye zahanati hizo inaanza kufanyika na kwamba hali ya huduma ni nzuri na Dawa zote muhimu zinapatikana kwa (asilimia 97)
 Nje ya Zahanati ya Buyango
Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala na Meneja wa MSD kanda ya Kagera na Geita Bwana Elgidius Rwezaura wakipokea maelezo kutoka kwa Muuguzi wa Zahanati ya Ruzinga Pascal Seko. 
Mganga wa Zahanati ya Ruzinga Edgar Rwegasira pamoja na wauguzi  Elzabeth Richard na Pascal Seko wakifatilia taarifa za ununuzi wa dawa kutoka kwa Elgidius Rwezaura wa MSD
Ukaguzi ndani ya Stoo ya Dawa ya Zahanati ya  Bulembo
Muuguzi wa Zahanati ya Bugorora pichani
Muonekano wa Majengo Zahanati ya Bugorora
Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dr.Deodorus Kamala akisalimiana na Wagonjwa waliofika kutibiwa kwenye Zahanati ya Buyango na kuwauliza upatikanaji wa huduma katika zahanati hiyo
Balozi Dr.Deodorus Kamala akiongea na wagonjwa waliofika katika Zahanati ya Buyango pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Vituo vya Afya na Zahanati Wilayani Missenyi.
Wakiagana na Wahudumu na wauguzi wa Zahanati ya Buyango
Muendelezo wamatukio ya picha Ziara ya Siku mbili ya Mbunge wa Jimbo la Nkenge Nkenge Balozi Dr.Deodorus Kamala#ZiaraBaloziKamala #VituovyaAfyanaZahanati
 Bango la Zahanati ya Kashanga iliyopo katika Kata ya Bwanjai
 #ZiaraBaloziKamala #VituovyaAfyanaZahanati

 Meneja wa MSD kanda ya Kagera na Geita Bwana Elgidius Rwezaura akiendelea kuwajibika
 #ZiaraBaloziKamala #VituovyaAfyanaZahanati
Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dr.Deodorus Kamala ametoa kiasi cha shilingi (milioni tano na laki sita ) 5,600,000/-kwa ajili ununuzi wa masanduku ya kubebea vifaa vya huduma ya kwanza (First Aid Kit) kwenye zahanati 10 za Halmashauri ya Missenyi,Masanduku hayo yakiwa na vitu muhimu vinavyohitajika kwa dharula mbalimbali.
Dr.Diodorus Buberwa Kamala amesema hayo alipofanya ziara katika Vituo vya Afya na zahanati kujionea changamoto na kuweka mikakati ya ufumbuzi katika huduma za Mama na Mtoto.Katika ziara hiyo ameongozana na Meneja wa MSD kanda ya Kagera na Geita Bwana Egidius Rwezaula .
Amezitaja Zahanati zilizopewa (First Aid Kit) ni Kashanga, Buyango, Bugandika,Kitobo, Kanyigo,Minziro ,Kyaka,Kilimilile,Bugorora pamoja na Kakindo .
Balozi Kamala amepongeza hali ya utoaji na ubora wa huduma za afya Wilayani Missenyi na kuwapongeza MSD kwa kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa huduma za Afya kupatikana .

Kwa upande wake Meneja wa Msd kanda ya Kagera na Geita Egidius Rwezaula amesema kuwa kazi ya kuyafikisha masanduku hayo kwenye zahanati hizo inaanza kufanyika na kwamba hali ya huduma ni nzuri na Dawa zote muhimu zinapatikana kwa (asilimia 97)
Muuguzi Zahanati ya Bulembo

Meneja wa MSD kanda ya Kagera na Geita Bwana Elgidius Rwezaura pichani kushoto akikagua list ya kiasi cha fedha waliyonayo Zahanati ya Kakindo Wilayani Missenyi. #ZiaraBaloziKamala #VituovyaAfyanaZahanati

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU