SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

27 August 2018

HALMASHAURI YA WILAYA MULEBA YABORESHA HUDUMA ZA AFYA VISIWANIAfisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza,Cornelia G.Mwillawi pichani kushoto akiongea na Mganga Mfawithi wa Zahanati ya kisiwani Mazinga ,Joanes Sweetbert muda mchache kabla ya kumkabidhi dawa ambapo amesema kuwa kwa sasa wilaya ya Muleba inapata dawa kwa asilimia 98 hivyo MSD watahakikisha maeneo yote hata yasiyofikika yanapata Dawa zote muhimu kwa asilimia 100%,Joanes Sweetbert ambaye ni Mganga Mfawithi ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kisiwa cha Mazinga pichani katikati.

Muonekano wa Mabosi yenye dawa yaliyonunuliwa kwa ajili ya Zahanati ya Mazinga o inahudumia visiwa vidogovidogi tisa (9) vyenye maelfu ya wananchi elfu na Serikali ya awamu ya tano kwa kushirikiana na MSD wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikisha huduma.
Dr. Modest Bateranisa Lwakahemula Burchard Mganga mkuu wa Wilaya ya Muleba akizungumza na wanahabari kuhusu changamoto na upatikanaji wa huduma za Afya.

Na Bukobawadau,Muleba
Halmashauri ya wilaya ya Muleba kupitia idara ya afya imenunua boti mbili na kuzisambaza katika visiwa vya Halmashauri hiyo ili kurahisisha huduma kwa wagonjwa wanaopata rufaa na kuletwa katika hospital zilizoko nchi kavu.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Dr. Modest Bateranisa Lwakahemula Burchardalisema kuwa kwa muda mrefu imekuwepo changamoto kubwa ya watu wanaoishi visiwani kuangaika na usafiri wa boti pale wanapozidiwa hali iliyokuwa inawalazimu wananchi kusubiri boti ya abria na kutumia gharama kubwa kukodi boti.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo Halmashauri imelazimika kununua boti na kuzisambaza katika maeneo muhimu ili akipatikana mgonjwa apate huduma ya haraka ambapo alisema kuwa boti nyingine kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa inatarajia kukamilika mwezi septemba na kuanza kutoa huduma ya kusafirisha wagonjwa
Wanahabari wakiendelea kumsikiliza Dr. Modest Bateranisa Lwakahemula Burchard Mganga mkuu wa Wilaya ya Muleba wakati anazungumzia changamoto na upatikanaji wa huduma za Afya Wilayani Muleba
Aidha alisema anaridhishwa na utendaji wa serikali katika swala zima la upatikanaji Dawa kwani kwa sasa upatikanaji dawa katika Halmashauri ya Muleba ni asilimia 98.
Hata hivyo aliwashukuru MSD kwa kusambaza dawa maeneo yasiyofikika hasa ya visiwani na kudai kuwa miaka michache iliyopita wananchi wa visiwani walipata matatizo makubwa kutokana na kutokewepo Dawa katika zahanath na vituo vya afya vilivyoko visiwani.

"Hakuna aliyetamani kuingia kisiwani kwani kunamabadiliko ya khali ya hewa lakini kwa utendaji wa MSD wao wanahakikisha huduma inatufikia kwa wakati na Dawa zinatoshereza ni jambo LA kujivunia na kumushukuru Mungu alisema Modest"

Awali akikabidhi dawa kwa Mganga mfawithi wa zahanathi ya kisiwa cha Mazinga afisa huduma kwa wateja kutoka MSD kanda ya Mwanza Cornelia G.Mwillawi alisema kuwa kwa sasa MSD wanahakikisha maeneo yote hata yasiyofikika yanapata Dawa muhimu kwa asilimia 100%
Alisema kuwa kinachotakiwa ni vituo hata vya visiwani kuleta oda za dawa zinazohitajika kwa mapema ili kuhakisha wananchi wanapata Dawa kwa wakati.
#Bukobawadau27Augosti2018

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU