SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

31 August 2018

MSD YAPELEKA HUDUMA WILAYANI NGARABohari ya Dawa Tanzania (MSD) kituo cha Muleba kinaendelea vyema kuwasogezea huduma za usambazaji wa dawa wateja wake Wilayani Ngara,Pichani Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (katikati), akiwakabidhi dawa na mifuko yenye vifaa vya kujifungulia wajawazito (Delivery Pack) wajumbe wa kamati ya afya wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Mifugo la Rusumo Wilayani Ngara mkoani Kagera jana. Kutoka kulia ni Koplo Apelius Kamugisha, Sajeni Scolastica Saganda na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya gereza hilo, Koplo Hashimu Bilalamo (kushoto)

Afisa Mahusiano Mwandamizi wa MSD Benjamini Massangya kushoto akibadilishana mawazo na Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (katikati) na Mfamasia wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Ndugu Patrick A.Ogo pichani kulia.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya gereza la Kilimo na Ufugaji la Rusumo Ngarahilo,Koplo Hashimu Bilalamo akiweka sahihi mara baada ya kukabidhiwa dawa hizo,kushoto ni Sajeni Scolastica Saganda Mjumbe wa kamati ya afya wa Jeshi Magereza wa Gereza la Rusumo.


Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya gereza hilo, Koplo Hashimu Bilalamo akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vua kutolea huduma za afya mkoani Kagera,Koplo Hashimu Bilalamo ametoa shukrani kwa ushirikiano wanaopata kutoka MSD na kupata huduma kwa wakati.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Rusumo, Flavian Joseph akiingiza dawa kwenye mtumbwi katika kivuko cha mto Luvuvu Wilayani Ngara tayari kwa kuvuka kuelekea katika zahanati husika.

Muendelezo wa tukio wakati Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Rusumo,Flavian Joseph na Mwenyekiti wa kamati ya afya wa zahanati hiyo, Emanuel Living wakiingiza dawa kwenye mtumbwi kivuko cha mto Luvuvui kuzipeleka katika zahanati hiyo

Taswira eneo la kivuko cha Mto Luvuvu Wilayana Ngara Mkoani Kagera.

Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi akimwelekeza sehemu ya kusahini muuguzi wa Zahanati ya Rusumo Lydia Samuel pichani kushoto


Muuguzi wa zahanati ya Rusumo, Lydia Samuel akiendelea kuwajibika wakati wa makabidhiano hayo

Muonekano wa Jengo la Zawahanati ya Rusumo Wilayani Ngara


Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kabanga , Juventh John akihesabu Dawa alizokabidhiwa

Bango la Zahanati ya Kabanga Wilayani Ngara

Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (kulia), akiwakabidhi dawa wafanyakazi wa Zahanati ya Kabanga. Kutoka kushoto ni Daktari wa zahanati hiyo, Abas Mwoseka, Muuguzi wa Zahanati hiyo, Esteria Julius na Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (kulia), akiwakabidhi dawa wafanyakazi wa Zahanati ya Kabanga. Kutoka kushoto ni Daktari wa zahanati hiyo, Abas Mwoseka, Muuguzi wa Zahanati hiyo, Esteria Julius na Mganga Mfawidhi, Juventh John mwenye tabasamu.

Bi Esteria Julius Muuguzi wa Zahanati ya Kabanga akiendelea kuwajibika


Baadhi ya Dawa zilizokabidhiwa Zahati ya Kabanga Ngara

Kaimu Meneja wa Mauzo wa Kituo cha Wilaya ya Muleba, Wasante Nyihirani wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vua kutolea huduma za afya mkoani Kagera.

Ndugu Wasante Nyihirani Kaimu Meneja wa Mauzo wa Kituo cha Wilaya ya Muleba alisema;Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) kituo cha Muleba kimesogeza huduma zake za usambazaji dawa mkoani Geita ili kuwapunguzia safari ndefu ya kwenda kupata huduma hiyo Kanda ya Mwanza. Kaimu Meneja wa Mauzo wa Kituo cha Wilaya ya Muleba, Wasante Nyihirani wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vua kutolea huduma za afya mkoani Kagera.

Alisema katika mkoa huo wilaya zilizonufaika na uanzishwaji wa kupeleka dawa Mkoani Geita ni Wilaya ya Mbogwe DC na Bukombe DC ambazo nazo imekuwa zikitoa huduma katika maeneo mengine ya mkoa huo.

#Bukobawadau #MsdTanzania


0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU