SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

28 August 2018

RUBYA MULEBA MAMA AJIFUNGUA WATOTO WATATU

BI Sajida Saidi 'Nyangoma' pichani Mkazi wa Kijiji Lubao kilichopo Kata ya Ijumbi Wilayani Muleba mkoani Kagera, amejifungua watoto mapacha wenye afya njema katika Hospitali Teule ya Rubya Wilayani Muleba.
Akizungumza na waandishi wa habari na timu ya maofisa wa Bohari ya Dawa MSD Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt.George Kasibante alisema hali ya mama huyo na watoto wake aliojifungua Jumapili Agosti 26,2018 inaendelea vyema.
"Watoto hawa waliozaliwa kabla ya muda wao wanaendelea vizuri na sasa wapo kwenye wodi maalumu ya joto" alisema Kasibante.
Alisema katika Hospitali hiyo ili ni tukio la pili kwa mama kujifungua watoto mapacha zaidi ya wawili kwani mwaka jana kuna mama mwingine alijifungua watoto watatu..
@mcbaraka akimjulia khali na kumpongeza Mama aliyejifungua Mapacha Watatu Katika hospitali Teule ya Rubya Wilayani Muleba  Bi.Sajida Saidi mkazi wa Kijiji cha Lubao Kata Ijumbi Muleba, watoto hao wamezaliwa wakiwa na uzito wa kilo 2.1,2.1 na 2.6 wakiwa na Afya njema
Mwanahabari Dotto Mwaibale akizungumza na Bi Shakira Saidi  ambaye ni pacha na Mama mzazi wa mapacha watatu Bi Sajida Saidi  (Nyangoma na Nyakato)
Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza,Cornelia G.Mwillawi pichani kushotoakiendelea kuwajibika,kulia ni Sr Theonestina John Muuguzi Mfawithi wa Hospitali teule ya Rubya.
 Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga cha 'Rubya Heath Training Institute' .
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa piliwa Chuo cha Uuguzi na Ukunga cha 'Rubya Heath Training Institute'
 Baadhi ya Wagonjwa waliofika kutibiwa katika Hospitali Teule ya Rubya Muleba leo Agosti 28 ,2018
 Diana Deusi mmoja wa wanahabari walioongozana na timu ya maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD)
Muonekano wa lango kuu la Hospitali Teule ya Rubya iliyopo Wilayani Muleba Mkoani Kagera. 

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU